Kukwama kwa
wajasiliamali katika sekta ya kilimo kushindwa kupata mikopo ya kifedha
kutoka taasisi za kibenki imetajwa kuchangiwa na vikwazo vinavyotokana
na changamoto ya ubora wa mazao yanayozalishwa na kupelekea kusababisha
ukosefu wa masoko hapa nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Kizimba Business Model uliofanyika katika viwanja vya SUGECO Morogoro,
Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Benki ya NMB - Isaac Masusu alisema kuwa
mijadala ilikuwa mingi ya njia ipi itakuwa bora kwa benki kuweza kutoa
mikopo ya muda mrefu katika sekta ya kilimo na sasa mfumo wa kilimo wa
Kizimba Business Model itakuwa imefungua njia ya kupata ufumbuzi wa
changamoto hiyo.
Masusu alisema kuwa mfumo huo unawezesha
vijana, akimama na wajasiliamali kuajiriwa katika sekta ya kilimo na
mpango huo umejikita katika uwezeshaji upatikanaji wa ardhi ambao
umekuwa kikwazo kikubwa kufanya shughuli za uzalishaji mali na kuongeza
thamani.
Masusu alisema kuwa moja ya kazi ya Benki ya NMB ni
kushirikiana na SUGECO katika kufungua njia kwa wakulima ili kuwezesha
kwa kushirikiana wadau wengine kufanya maeneo yanayosababisha mabenki
kushindwa kutoa mikopo ya kilimo kwa makundi hayo kuwepo na suluhu.
Benki
ya NMB kwa sasa itaanza kutoa mikopo ya muda mrefu ambayo wakulima
watanufaika nayo kutokana na aina ya uwekezaji katika sekta ya kilimo,
inayohitaji fedha nyingi na kwa muda mrefu, alisema Masusu.
Naye
Waziri wa Kilimo - Profesa Adolf Mkenda alisema kuwa Sekta ya kilimo
imekuwa ikiajili nguvu kazi nyingi hapa nchini lakini imekuwa haina
tija- akitolea mafano zao la mchikichi nchini ya Indonesia na nchi
nyingine duniani limekuwa na faida kubwa tofauti na Tanzania.
“Indonesia
kwa hekta moja hupata tani 10 ya mafuta ya mawese wakati Tanzania hekta
moja tumekuwa tukipata mafuta ya mawese tani 0.6, ni dhahiri kuwa
lazima tuboreshw kilimo chetu ili kilete tija”alisema Profesa Mkenda.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro, Profesa
Raphael Chibunda alisema kuwa chuo hicho ni wadau wakubwa wa Sekta ya
Kilimo na kupitia SUGECO imefanya mabadiliko na mageuzi makubwa kwa
wanafunzi kujifunza zaidi.
Waziri wa Kilimo - Profesa Adolf Mkenda akionyeshwa mkate uliokwa kwa unga wa viazi lishe na Mkurugenzi Mtendaji wa Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO), Revocatus Kimario wakati wa kuzindua mfumo wa Kizimba Business Model, Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki - Dismas Prosper.
Mkuu
wa Kitengo cha Kilimo na Biashara wa Benki ya NMB -Isaac Masusu
akizungumza wakati wa uzinduzi wa muongozo wa mfumo wa Kizimba Business
Model unaolenga kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara nchini
mkoani Morogoro.
Waziri
wa kilimo, Profesa Adolf Mkenda akiangalia bidhaa za vyakula lishe
vilivyozalishwa na Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative
(SUGECO) kabla ya kuzindua mfumo wa Kizimba Business Model unaolenga
kuwaunganisha vijana kufanya kilimo biashara nchini mkoani Morogoro
akishuhudia ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Mashariki - Dismas
Prosper (wa kwanza kushoto).
Friday, March 19, 2021
NMB Yatoa Neno Katika Uzinduzi Kizimba Business Model – Morogoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment