Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya weka ushinde Bonge la Mpango inayoendeshwa na Benki ya NMB. Kushoto ni mwakilishiki kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na kulia ni Afisa Huduma kwa wateja wa benki ya NMB, Neema Deusi.
…………………………………………………………………………….
Droo ya kwanza ya Kampeni ya Weka Akiba na Ushinde inayoendeshwa na Benki ya NMB iitwayo Bonge la Mpango, imefanyika ambako washindi 10 wameshinda pesa taslimu na wawili wakijitwalia pikipiki ya tairi tatu aina ya Lifan Cargo.
NMB Bonge la Mpango, inalenga kutambua na kuthamini utamaduni chanya wa wateja kujiwekea akiba, ikiwa ni pamoja na kurejesha sehemu ya faida ya benki hiyo kwa mwaka uliopita, ambako NMB ilipata faida ya zaidi ya sh. Bilioni 205.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Ally Ngingite, aliwataka wateja wa benki hiyo kuendelea kujiwekea akiba mara kwa mara, ili kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya sh. Milioni 550
Ngingite alibanisha kuwa, ukiondoa pesa taslimu wanazoshinda wateja wa kila wiki, NMB Bonge la Mpango pia inawawezesha wateja wawili wa kila wiki kushinda pikipiki ya mizigo, gari dogo la mizigo aina ya Tata ‘Kirikuu’ na Toyota Fortuner.
“Ukiweka kuanzia Sh. 100,000 anakuwa na nafasi ya kushinda pesa taslimu, pikipiki ama kirikuu na wale ambao akaunti zao zitakuwa na akiba isiyopungua Sh. Milioni 10, watashindania Toyota Fortuner ya Sh. Mil. 169,” alisema Ngingite.
Kwa upande wake, Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Elibariki Sengasenga, aliipongeza NMB kwa kampeni zilizobeba uwezeshaji kwa wateja, huku akiwahakikishia washiriki kuwa droo hizo zinafuata taratibu zote. Lakini pia aliwahakikishia wateja kuwa hakuna ubabaishaji wowote. washindi watapatikana kutokana na bahati zao tu na si vinginevyo, hivyo wawe huru kushiriki na watashinda,” alisema Semasenga.
Washindi wa LIFAN Cargo ni Martha Mathew Mmasi wa Dar es Salaam na Willy Moses Mwasaka wa Tukuyu.
No comments:
Post a Comment