Airtel Tanzani imetangaza kuiingia ubia na Benki ya TPB kwa lengo na dhamira ya kuboresha na kupanua wigo wa huduma za kifedha nchni Tanzania, Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money imekua ikitoa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwemo kutoa na kupokea pesa popote, kulipia Ankara mbalimbali kama vile LUKU, DSTV, malipo mbalimbali ya serikali, huduma za Maji kama Dawasco na nyingine nyingi .
Akiongea wakati wa Mkutano maalum na waandishi wa habari wakutangaza Ubia kati ya Airtel na TPB benki, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema “Ubia tunaoingia hapa leo utasaidia sana kuboresha huduma tunazotoa kwa kuwafaidisha zaidi mawakala wetu wa Airtel Money waliopo kila mahali nchini ambapo benki ya TPB imefika.
Pia Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika kabisa wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali.
Nchunda
alielezea kuwa “Mawakala sasa hawana haja ya kubeba bulungutu la fedha
na kusafiri umbali mkubwa kupata salio au (Float), sasa watahudumiwa
kwenye tawi lolote la TPB karibu yake, Hii itasaidia sana kwenye kuokoa
muda na fedha ambazo walizitumia kama nauli kwenda umbali mrefu ili
kupata salio/Float, sasa ni haraka zaidi na salama. Ubia wetu na Benki
ya TPB unalengo la kuendeleza ubunifu katika utoaji wa huduma za fedha
kiditali kwa kupunguza madhara yanayowakumba mawakala au wateja wetu
wanaposafiri umbali mrefu kufata huduma, sasa watajiunga na benki ya TPB
karibu yao na kufanya miamala yote kigitali kupitia Airtel Money kwenda
benki au kutoka benki kwenda Artel Money.
Muunganiko wetu utaendelea kukamilisha dhamira yetu tuliyojiwekea sisi wabia ya kutoa huduma nafuu, kwa haraka, bila mipaka ili kikidhi mahitaji ya wateja wetu ya kila siku alisisitiza Nchunda Akiongea kwa niaba ya TPB benki Mkurugezi wa huduma za kimtandao Bw, Jema Msuya alisema “TPB tunaaamini suluhisho la huduma za kifedha katika utoaji huduma unatija sana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, hivyo basi Ubia wetu na Airtel ni muendelezo wa kuendelea kupunguza changamomoto za pande zote yaani za wale waliofikiwa na huduma za kibenki na ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki popote walipo kwa kuwa sasa watapata huduma kwa njia ya mtandao na kufanya malipo kidigitali.
“Benki
ya TPB kila tuponakuja na huduma yenye ubunifu zaidi lengo letu ni
kuongeza au kutoa suluhisho zaidi kwa wateja wetu pamoja na kuwapatia
huduma kwa unafuu huku tukizingatia ubora zaidi. Ubia wetu na Airtel
Money leo hii unadhihirisha dhamira yetu hiyo ya kutoa huduma kabambe,
zenye usalama bila kuzingatia mipaka yaani huduma popote ulipo. Kila
mteja wetu anaweza kujipatia huduma zetu akiwa na simu yake kiganjani
kutokana na ubia huu sasa.” Alisema bw, Msuya .
Ili
wakala wetu au Mteja aweze kupata huduma hii ya atatakiwa kutembeleia
tawi letu la TPB bank na kujaza fomu maalum ya huduma bila kupoteza
wakati ataanza kufurahia huduma zetu kwa kupiga *150*60# cahagua namba 0
Ongeza Pesa
Select 2 Hamisha toka Benki
Select 4 TPB Benki na ufuate Maelekezo.
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda (kulia) na Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki wakionyesha bango baada ya kuzindua ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali.
Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki akiongea jijini Dar es Salaam wakati akitangaza ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali. Kulia ni Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda akiongea jijini Dar es Salaam wakati akitangaza ubia baina ya Airtel ba Benki ya TPB ambapo Wateja wa Airtel Money sasa watakuwa na uhakika kufanya miamala yao kwa uhakika wakiwa popote kama vile kuhifadhi au kutoa pesa toka benki ya TPB kwenda moja kwa moja kwenye akaunti zao za Airtel Money ili kufanya malipo mbalimbali ya huduma kama vile LUKU, Ankara za Maji, DSTV, au kukamilisha malipo mbalimbali ya tozo za serikali. Kushoto ni Mkurugezi wa huduma za kimtandao Jema Msuya kutokaTPB benki.
No comments:
Post a Comment