HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 10, 2021

WANANCHI MTAA WA MBOPO WAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YAO

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni, Mohamed Bushir akizungumza na wazazi, walezi  leo  tarehe 9 Februari 2021.  katika mkutano  wa kujadili masuala mbalimbali kuhusina na maendeleo ya shule, mkutano  ulifanyika katika  viwanja vya shule ya Sekondari  ya Mbopo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni, Mohamed Bushir akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalim Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbopo,Jackson Mlinda akisoma hotuba yake katika mkutano huu uliofanyi tarehe 9 Februari 2021 kwenye viwanja vya shule hiiyo

(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Na Mwandishi wetu, Michuzi TV
WANANCHI wa Mtaa wa Mbopo uliopo Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wamekutana kwenye kikao cha kuweka mikakati na mipango ya shuleta na maedeleo katika mtaa wao huku wakitumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge wao kutoka Jimbo la Kawe,Askofu Josephat Gwajima kwa kutimiza ahadi yake kwa kuwapatia gari.

Wakizungumza leo wakati wa kikao hicho ambacho kimefanyika katika Shule ya Sekondari Mbopo wametumia nafasi hiyo kuzungumzia namna ambavyo wamejipanga katika kuhakikikisha wanapata maendeleo.

Pia wamezungumzia mikakati ya wananchi ambavyo wanaweza kushirikiana na uongozi wa Shule ya Sekondari Mbopo kutatua baadhi ya changamoto zilizopo.

Akizingumza na Michuzi TV, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo,Mohamed Bushir amesema kwamba wamekutana leo kwenye kikao ambacho kimewashirikisha wananchi kwa ajili ya kujadili mipango na mikakati ya maendeleo ya shule yao pamoja na mtaa wao.

"Tulikuwa nachangamoto kubwa ya usafiri ambayo ilikuwa inawakabili wananchi wetu, hasa kutoka Mabwepande, Bunju mpaka Mbopo mpaka kuiapata Madale na Nyuki .Lakini tayari tumefanya mawasiliano na Diwani wa Kata yetu na ametueleza ameshafanya mawasiliano na Mbunge wetu Askofu Gwajima ambaye ameshakabidhi gari.

"Tunamshukuru Mbunge kwa kutatua changomoto ya usafiri, ni changamoto ya muda mrefu, bahati nzuiri miundombinu ya barabara iko vizuri kwani iko kwa kiwango cha changarawe na tayari Serikali imeanza mkakati wa kujenga baadhi ya barabara zetu kwa kiwango cha lami,"amesema Bushir na kusisitiza kupitia kikao hicho wamejadilia mambo mengi ya maendeleo ya mtaa wao.

Kwa upande wake Mwalim Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbopo Jackson Mlinda amesema katika kikao hicho wamezungumzia maendeleo ya shule hiyo na kikubwa ambacho wamekiomba kutoka kwa wazazi na walezi ni ushirikiano ili kutimiza yale ambayo wamekubaliana katika kikao hicho.


"Tukishirikiana kwa umoja wetu , tutapiga hatua ya maendeleo kwa haraka zaidi, hivyo tunawaomba wazazi tulichokubaliana basi tutimize kwa pamoja,"amesema.

Wakati huo huo mwananchi Philip Mushi ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli kwa kutoa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari kwani kwa kufanya hivyo imewapunguzia mzigo wananchi.

Aidha Mwamvita Juma ambaye ni miongoni mwa wananchi wa mtaa huo ametoa ombi kwa Serikali kuhakikisha mabweni ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Mbopo yanakamilika kwani hivi sasa wanalipa Sh.milioni 1.2 kwa mwaka kulipia gharama za hosteli.

"Tunaomba Serikali isimamie hosteli ya shule iishe ili wanafunzi waweze kukaa shuleni ili kuondoka na gharama kubwa ambayo wazazi tunalipa, kila mwezi tunalipa Sh.100,000,"amefafanua.

Kwa upande wake Rehema Msola amemshukuru Rais Magufuli kwa kutoa elimu bure, kwani amewakwamua watu wa chini.Pia ametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la KaweAskofu Josephat Gwajima kwa kuwapelekea usafiri kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya usafiri.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad