WAAJIRI watakiwa kuhakikisha wanaangalia maslahi ya wafanyakazi kwa kuwaajiri, kuzingatia haki na usalama kazini ili maendeleo endelevu yawepo. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 13, 2021

WAAJIRI watakiwa kuhakikisha wanaangalia maslahi ya wafanyakazi kwa kuwaajiri, kuzingatia haki na usalama kazini ili maendeleo endelevu yawepo.

 

Hayo yamesemwa leo na Mwanasheria kutoka Kituo cha Misaada wa Sheria kwa Wanawake  na Mratibu Uwezeshaji jamii kwenye masuala ya haki na sheria na ajira hususan kwa makundi ya vijana na wanawake, (WLAC) Consolata Kikoti wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na za umma ili kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao jijini Dar es Salaam.

Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la uelewa wa sheria na haki za wafanyakazi zinazokiukwa.

Changamoto nyingine ni usimamizi na utekelezaji wa sheria, kutokuwepo uwajibikaji katika kuhakikisha sheria hizo zinatekelezwa hasa katika taasisi.

Pia amesema vyama vya kutetea wafanyakazi vinatakiwa kusimamia haki hizo.

"Mafunzo haya ya siku moja yaliyoandaliwa na kituo cha  msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) yamewashirikisha Chama cha waajiri na wadau wanaohusika na masuala ya wafanyakazi na lengo ni kuwaweka pamoja kuona namna watakavyowasaidia wafanyakazi na kusimamia haki za wafanyakazi katika maeneo yao," amesema Kikoti.

Naye, Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Ilala, Vicky Kibona amesema haki za wafanyakazi zifuatwe kwani waajiri wamekuwa wakiwaachisha wafanyakazi bila kufuata utaratibu.

Amesema sheria za msingi zinazosaidia mwajiri kumsimamisha mfanyakazi au mfanyakazi kuacha kazi ni  sheria ya ajira na mahusiano kazini.

"Waajiri wafuate utaratibu endapo wanataka kuahirisha kazi kwa mwajiriwa au kumsimamisha ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza," amesema Kibona.

"Wafanyakazi wengi wanaachishwa bila kufuata utaratibu na imesababisha kuwa na kesi nyingi mahakamani hivyo, ni  lazima kufuata utaratibu wa kumwachisha mfanyakazi anapokuwa kazini kupata haki zake na  kupunguza kuongezeka kwa kesi hizo," amesisitiza Kibona.

Windi Clement ambaye ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi SS Tanzania Limited amesema mafunzo hayo yatamsaidia kuboresha mahusiano mema kwa wafanyakazi na waajiri na kutetea wafanyakazi kuhakikisha wanapata haki zao.

Amesema viwanda vingi vinachangamoto ya mikataba kwani asilimia kubwa hutoa mikataba ya mwaka mmoja hivyo, haiwapi nguvu wafanyakazi kuweza kupambana kufanya kazi za uzalishaji.

Pia amesema uwepo wa kampuni tanzu ndani ya kampuni moja husababisha kukosekana kwa uwakilishi wa vyama vya wafanyakazi na hivyo, kusababisha wafanyakazi wengine kunyanyasika.

Mwanasheria kutoka kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Mratibu Uwezeshaji jamii kwenye masuala ya haki, sheria na ajira hususani kwa makundi ya vijana na wanawake, Consolata Kikoti akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi kuwajengea uwezo wa kutambua haki zao yaliyotolewa na WLAC leo Februari 12, 2021 jijini Dar es Salaam
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Ilala, Vicky Kibona,akizungumza na waandishi wa habari namna mafunzo kwa wafanyakazi kutambua haki zao za ajira kazini yatakavyokuwa na manufaa kwao.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali binafsi na zile za umma wa wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo kutambua haki zao leo jijini Dar es Salaam.
Bundi Clement, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi kiwanda cha Pepsi nchini, akizungumza baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ya siku moja kwa wafanyakazi wa a sekta binafsi na Umma ya kuwajengea uwezo kutambua haki zao za yaliyotolewa na WLAC  leo Februari 12, 2021  jijini dar es Salaam.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad