HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 10, 2021

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA SEKTA YA NGUO NA MAVAZI NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZAO

 


NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe  amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta hiyo.      
         
Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika  Februari 9, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE ) jijini  Dodoma Naibu Waziri amewaagiza kuwasilisha changamoto walizonazo na rasimu za mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.

Katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto na mapendekezo yao kwa Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la ndani la bidhaa hizo pamoja na kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to Clothing Strategy C2C 2016 - 2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 - 2032.

Baadhi ya waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  Exaud Kigahe (hayupo pichani)  katika kikao kilichofanyika 9 Februari 9, 2021 jijini  Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akiongea na wadau wa Sekta ya  Nguo na Mavazi alipokutana nao ili ksikiliza changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na  mavazi nchini kwenye kikao kazi cha pamoja Februari 9, 2021 jijini  Dodoma.
Baadhi ya waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  Exaud Kigahe (hayupo pichani)  katika kikao kilichofanyika 9 Februari 9, 2021 jijini  Dodoma.
 




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad