HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 1, 2021

MWAISUMBE AOMBA UWEPO WA MAWAKILI MAHAKAMA ZA MWANZO

 


Jane Edward, Michuzi TV- Arusha

MKUU wa wilaya ya Longido ,Frank Mwaisumbe ameiomba serikali kuwepo kwa mawakili katika mahakama za mwanzo ili wasaidie wananchi kutambua haki zao za msingi kabla ya kesi zao kufika mahakamani.

Aliyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,Idi Kimanta wakati akizungumza katika siku ya maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini iliyofanyika mahakama kuu mkoani humo.

"tumekuwa tukipokea malalamiko mengi Sana kutoka kwa wananchi wakilalamikia kudhulumiwa haki zao na kuona hawajatendewa haki na mahakama ,lakini kungekuwepo na mawakili katika mahakama hizo ingesaidia sana kupatiwa elimu na kueleweshwa haki zao zilivyo."alisema Mwaisumbe.

Jaji mfawidhi wa mahakama kuu Kanda ya Arusha, Moses Mzuna alisema mahakama zinatakiwa kutenda kazi ya msingi ya kutoa haki bila vishawishi,vitisho au kuingiliwa na mtu au mhimili mwingine au kupewa ahadi fulani ili kutoa maamuzi ya kupendelea upande huo.

"Msingi wa udugu umejikita zaidi katika kuchukuliana ,kwamba pamoja na udhaifu wa watoa uamuzi mahakimu,majaji na hata wasaidizi wao,tusilaumu chombo cha mahakama bali tukisaidie kutimiza malengo yake ya kutoa haki sawa na kwa wakati,na mtu asiporidhika na uamuzi anashauriwa kukata rufaa mahakama ya juu."alisema Jaji mfawidhi.

Naibu Msajili mfawidhi mahakama kuu Arusha, Ruth Massam alisema kuwa,katika kuadhimisha wiki hiyo ya sheria mahakama na wadau wametoa elimu ya sheria sehemu mbalimbali zikiwepo , Ilboru sekondari,Matevezi ,shule ya msingi Naurei,na kutoa elimu kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Ruth alisema kuwa, shughuli hizo za kutoa elimu ya sheria zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani wananchi wengi wamejitokeza na matatizo yao kutatuliwa hapohapo na wengine wameelekezwa sehemu wanakoweza kwenda ili matatizo yao yatatuliwe.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad