MKUU WA SHULE AVULIWA MADARAKA KWA KUSHIDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 19, 2021

MKUU WA SHULE AVULIWA MADARAKA KWA KUSHIDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

 Na Woinde Shizza, Michuzi Tv-Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha,  Iddi Hassan Kimanta amemwagiza afisa elimu Mkoa, Halfan Omari Masukira kumvua madaraka ya ukuu wa shule mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Irkaswa, Arbogastus Mushi na mwalimu wa taaluma kwa kushindwa kusimamia ufundishaji katika shule hiyo iliyopo Wilayani Longido.

Maelekezo hayo ameyatoa alipokuwa akizungumza katika kikao na Maafisa Elimu kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha, Kikao kilichofanyika Katika ukumbi wa jengo la mkuu wa mkoa Arusha.

Kimanta amesema ni aibu kubwa sana kwa mwalimu mkuu kutohakikisha vipindi vyote vinafundishwa na walimu wake kwa wakati.

“Hii inaashiria ni usimamizi mbovu wa mwalimu mkuu na mwalimu wa taaluma, kwani wanafunzi wamekuwa wakifundishwa masomo machache kwa siku huku mwalimu mkuu hajui chochote.” Alisema.

Amewataka maafisa elimu hao kwenda kuwasimamia walimu wakuu wa shule kwa ukaribu zaidi, kwani Mkoa wa Arusha unasifa ya kushika nafasi nzuri katika matokea ya mitihani mbalimbali, hivyo baadhi ya walimu wakuu wasikwamishe jitihada hizo.

Nae, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha David Lyimongi, amemuagiza Afisa Elimu mkoa, bwana Masukira kuhakikisha miongozo yote inayoletwa kutoka TAMISEMI iwe inaendana na uhalisia wa hali ya sasa ili sekta ya elimu iendelee kuimarika zaidi.

Mkoa wa Arusha umekuwa ukifanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa na kwa mwaka 2020 kidato cha sita Mkoa ulishika nafasi ya 7 Kitaifa, kidato cha nne nafasi ya 1, kidato cha pili nafasi ya 1, darasa la saba nafasi ya 2 na darasa la nne nafasi ya 3.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad