Na Amiri Kilagalila, Njombe
CHAMA kikuu
 cha ushirika mkoani Njombe (NJORECU) kinatarajia kuanza upya uchakataji
 wa unga wa mahindi kupitia kiwanda kinachomilikiwa na Chama hicho 
kilichosimama mwaka 2019 ikiwa ni miezi tisa baadaye mara baada ya 
kufunguliwa na kuanza kufanya kazi mwaka 2018.
Meneja
 mkuu wa NORECU mkoa wa Njombe Samuel Mlumba,amebainisha hayo katika 
mkutano na wanachama uliofanyika mjini Njombe,huku akibainisha kuwa zipo
 sababu mbali mbali ikiwemo changamoto za uongozi zilizosababisha 
kiwanda hicho kufanya kazi kwa muda mfupi na kutokana kuondoshwa kwa 
changamoto hizo hakuna sababu itakayozuia kiwanda hicho cha uchakataji 
wa Sembe kuanza kufanya kazi.
Mlumba
 amesema Kiwanda  kilichopo mjini Njombe  kilichosimama March 2019 huku 
kikiwa kimefanya kazi miezi 9 tangu kilipoanza kufanya kazi June 2018 
kinatarajiwa kuanza uzalishaji kuanzia June mpaka March mwaka wa fedha 
wa 2022
“Sababu
 zilizopelekea kufanya kazi kwa miezi 9 safari hile sasa hivi 
hazipo,kwasababu zilikuwa ni changamoto za kiutumishi na usimamizi wa 
kiwanda hicho”alisema Mlumba
Aliongeza
 “Tupo kwenye mkakati wa kutafuta wataalamu waweze kututengenezea mpango
 biashara kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata Sembe”aliongeza Mlumba
Nestory
 Betram ni kaimu mhasibu mkuu wa NJORECU,amesema kabla ya kufika mwaka 
wa fedha wanatarajia kununua tani za mahindi 1199.7 zenye tahamani ya 
shilingi milioni 600 kutoka kwenye AMCOS mbali mbali.
Benedict
 Mwageni ni Mwenyekiti wa bodi ya mpito wa chama kikuu cha ushirika mkoa
 wa Njombe,ametoa wito kwa wakulima walioko kwenye AMCOS kujiandaa 
kunufaika kwa kuwa kiwanda hicho kinaenda kuongeza thamani ya mazao.
“Soko
 la kwanza la mahindi la wana Njombe liwe ni Chama kikuu cha ushirika, 
kiwanda chetu kitakapoanza kufanya kazi,tunatarajia kila siku kuchakata 
Mahindi tani zisizokuwa pungufu ya 15 kwa hiyo kwa mwaka tutakuwa na 
kilo 4500”alisema Benedict Mwageni
Romanus
 Lugome na Mariana Chaula ni miongoni wa viongozi wa vyama vya msingi 
(AMCOS) mkoani Njombe wameshukuru uongozi wa Chama Kikuu kuona namna ya 
kufufua matumaini ya muda mrefu ya Chama kundeleza miradi yao ikiwemo 
kiwanda hicho kitakachokuwa na msaada kwa wakulima wa Mahindi.
 Samuel
 Mlumba Meneja mkuu wa NORECU mkoa wa Njombe akieleza namna 
walivyojipanga kuendeleza miradi ya Chama ikiwemo uendeleaji wa eneo 
lililopo kata ya Mlangali wilayani Ludewa lililotengwa kwa dhumuni la 
kujenga kiwanda kingine cha kuchakata Sembe mkoani Njombe.
Baadhi
 ya viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) Katika mkutano mkuu wakiwa 
makini kusikiliza ajenda ya fedha na mipango ya Chama kikuu ili 
kuimarisha ushirika mkoani humo.
Moja
 ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata mahindi kinachomilikiwa na NJORECU 
kilichopo kata ya Njombe mjini wakati kilipoanza kufanya kazi.


No comments:
Post a Comment