Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu(kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu namna Benki hiyo
ilivyoshiriki kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa Kansa wakati
wa maadhimisho ya kansa Duniani yanayofanyika kila tarehe 04 mwezi Februari kila mwaka. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu.
Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu
akitoa ufafanuzi baadhi ya mambo yanayohusu benki hiyo wakati wa mkutano
na waandishi wa habari waliofika makao makuu ya Benki hiyo iliyopo
Kinondoni jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya Ecobank Tanzania, Charles Asiedu.
ECOBANK Tanzania kwa kushirikiana na taasisi na asasi za kiraia ikiwemo Kampuni ya Chief Promotions wameungana katika kutoa elimu ya uelewa kwa Serikali na Umma wa watanzania pamoja na kutoa misaada ya vifaa vya shule,Vipima Joto, Maziwa ya Unga,Sabuni, Pampasi, Dawa za meno, miswaki pamoja na Mafuta ya Kupaka kwa Watoto wenye matatizo ya Kansa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Kansa
duniani Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Ecobank Tanzania, Charles
Asiedu ameeleza kuwa saratani hukatiza maisha ya maelfu ya watanzania
kila mwaka na benki hiyo imeendelea kutoa elimu ya uelewa kuhusiana na
magonjwa yasiyoambukiza kupitia kampeni yao ya miaka mitatu ambayo kwa
kiasi kikubwa wametoa elimu ya Afya na kubadili mitindo ya maisha.
"Kupitia
kampeni yetu ya Kupambana na magonjwa yasiyoambukiza Ecobank tumekuwa
tukihimiza kuzingatia chakula bora, kufanya mazoezi, kutovuta sigara na
kupunguza unywaji wa pombe." alisema Asiedu .
Amesema kuwa katika maadhimisho ya uelewa katika siku ya saratani
duniani Ecobank itafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa msaada wa
watoto waliothirika na saratani katika hospitali ya taifa Mhimbili
pamoja na kutoa jumbe mbalimbali za uelewa wa kansa kupitia Televisheni,
Redio na mitandao ya kijamii ili kujenga uelewa zaidi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko katika Benki hiyo, Furaha Samalu
amesema wataendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa huo, kuelimisha Jamii na
kuhimiza Jamii kula Milo ya Kiafya ili kujikinga na maambukizi ya
Kansa.
“Sisi
tunafahamu Ugonjwa wa Kansa ni zaidi ya Ukimwi, Malaria na hata
COVID-19, hivyo sisi tunawapenda Watanzania wote na watu wote duniani
wachukue tahadhari kujinga na Kansa”, amesema Samalu.
Tafiti
zinaonesha kuwa watu milioni kumi hufariki kwa tatizo la saratani kote
ulimwenguni huku ikielezwa kuwa vifo hivyo ni zaidi ya vile
vinavyosababishwa na UKIMWI na Malaria, na inakadiliwa kuwa hadi kufikia
2030 vifo vitikanavyo na saratani vitafikia milioni 13 kama hatua
madhubuti hazitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment