Katibu
Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainabu Chaula
amelitaka baraza la wafanyakazi wa shirika la posta Tanzania kufanyakazi
kwa weledi na kuweka mikakati ya kuhakikisha shirika hilo linajiendesha
kwa faida na kuchangia uchumi wa taifa.
Dkt Chaula ameyasema
hayo Jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi
wa shirika la posta nchini waliokutana kujadili na kutathmini utendaji
kazi wa shirika hilo katika utendaji kazi wake.
Amesema ni wajibu
wa kila mtumishi ndani ya shirika hilo kuhakikisha anafanyakazi kwa
bidii na kuongeza tija katika shirika na kuongeza uzalishaji kama
ilivyokusudiwa wakati wa uanzishwaji wa shirika hilo.
“Kila mtu
ndani ya shirika ajitathmini amelifanyia nini shirika, kila taasisi
imewekewa target ataongeza vipi ajira mpya za ndani kama nchi
tumejiwekea ajira milioni nane 8,000,000 kati ya hizo je taasisi yako
itatoa ngapi” amesema Dkt Zainabu Chaula.
Aidha Dkt.Chaula
amelitaka shirika kujitathmini katika utendaji kazi wao katika Mkoa yote
kuhakikisha Mikoa yote inafanya vizuri na kusaidia Mikoa ambayo
haifanyi kazi vizuri ili nayo ifanye kazi vizuri.
Dkt.Chaula
amesema kuwa kwa sasa utendaji kazi wa shirika unazidi kuimarika hivyo
kila mtumishi kuhakikisha anafanya kazi kwa bidii ili kuendelea
kuboresha zaidi huduma zinazotolewa na shirika la posta.
Aidha
amewataka wajumbe wa baraza kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata juu ya
huduma mpya zilizoanzishwa na shirika na kuongeza mchango katika kukuza
uchumi wa nchi kupitia sekta ya mawasiliano.
Awali Posta masta
Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe amesema baraza
limekaa kwa siku tatu (3) likishirikisha watumishi kutoka ngazi
mbalimbali kwa lengo la kutathmini na kuweka malengo katika kuimarisha
utendaji kazi wa shirika la posta.
Aidha katika siku tatu hizo
walipata wasaa wa kuchagua viongozi mbali mbali wa baraza na kupata
mafunzo ya viashiria vya hatari katika uzalishaji wa shirika na kukuza
uchumi wa nchi na utunzaji wa nyaraka za shirika.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi ,akizungumza wakati wa kufunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
Posta masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe,akielezea jinsi walivyojifunza mafunzo hayo kwa siku tatu wakati wa kufunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainabu Chaula (hayupo pichani) wakati akifunga kikao cha baraza la 27 la wafanyakazi wa shirika la posta nchini kilichofanyika siku tatu jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment