HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 25, 2021

CRDB TAWI LA KARIAKOO-NARUNG’OMBE WAPOKEA MZIGO ULIOBORESHWA

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kariakoo - Narung’ombe jijini, Holo Buyamba akitoka neno la shukrani kwa wateja wa Benki hiyo na wafanyakazi wakati wakipokea na kusheherekea Mzigo mpya ulioboreshwa.

 

Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya CRDB, Tawi la Kariakoo - Narung’ombe wakijumuika kwa pamoja kupokea Mzigo Mpya ulioboreshwa katika Tawi hilo jijini Dar es Salaam.


Wafanyakazi na Wateja wa Benki ya CRDB, Tawi la Kariakoo - Narung’ombe wakijumuika kwa pamoja kupokea Mzigo Mpya ulioboreshwa katika Tawi hilo jijini Dar es Salaam.

 

****************************

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

Benki ya CRDB Tawi la Kariakoo - Narung’ombe imepokea huduma mpya SimBanking iliyoboreshwa kwa ajili ya matumizi ya Wateja wake.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Salaam, Meneja wa Tawi hilo, Holo Buyamba amesema wateja wa Benki hiyo wanaweza kufanya huduma za Kibenki na kuendelea kufurahi huduma hizo akiwa sehemu yoyote baada ya maboresho hayo yaliyofanyika.

“Zamani kufungua Akaunti zilikuwa zinahitajika nyaraka nyingi lakini sasa hivi Kitambulisho cha Utaifa kinakupa Akaunti yako bila kutembelea Tawi la Benki, pia kulipa Bili mbalimbali popote pale bila kwenda tawi la benki”, amesema Buyamba

Buyamba amewakaribisha Watanzania kuchangamkia fursa kujiunga na huduma hiyo, pia amesema kwa wale waliojiunga wapakue upya App ya SimbBanking ili kuendelea kutumia Mzigo mpya ulioboreshwa.

Kwa upande wake, Mteja wa Benki hiyo, Abdul Rugambwa amesema wanafurahia ujio wa huduma hiyo mpya iliyoboreshwa kwa kuwa itawasaidia kurahisisha shughuli mbalimbali bila kufika matawini kupata huduma hizo za Kibenki.

“Itatusaidia kufanya huduma mbalimbali za Kibiashara kwa sisi Wafanyabiashara tutaweza kupata huduma hata tukiwa nyumbani au sehemu yoyote, kwa kweli tunawashukuru CRDB na mzidi kuboresha huduma”, ameeleza Rugambwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad