ALIYETELEKEZWA NA MUME KISA MTOTO MWENYE ULEMAVU ASAIDIWA NA MERIDIAN BET - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 1, 2021

ALIYETELEKEZWA NA MUME KISA MTOTO MWENYE ULEMAVU ASAIDIWA NA MERIDIAN BET

Na Mwandishi wetu
SIKU chache zilizopita baada ya baadhi ya vyombo vya habari kufanya kipindi na Zuhura Shabani (32) ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja aliyetelekezwa na mume wake kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ulemavu wa mtoto wake hatimaye apewa msaada na MERIDIAN BET

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Mkuu wa Utawala wa kampuni ya michezo ya kubashiri MERIDIAN BET Cornelius Boenman amesema kampuni yao imekuwa ikishiriki katika jamii kwa lengo la kuwasaidia wenye uhitaji.

Naye Meneja ustawi wa MERIDIAN BET Amani Maeda amesema wao kama kampuni wameguswa na matatizo aliyonayo Zuhura Shabani hivyo wakaamua kumsaidia mtaji wa biashara.

Kwa upande wake Zuhura ameishukuru Kampuni ya Meridian Bet kwa msaada huo ambapo amesema utasaidia kumuwezesha kufungua saluni ya kike ambayo iasaidia kumlea yeye pamoja na mtoto wake.

‘Naishukuru sana Kampuni ya Meridian Bet kwa moyo mlioonesha wa kunisaidia kiasi hiki cha pesa, naahidi pesa hii mliyonipatia nitaitendea haki, nitafungua Saluni kama nilivyosema najua saluni itanisaidia kuendesha maisha yangu na mwanangu na kunipunguzia kutembea mtaani na kuomba omba msaada, Mungu awabariki muendelee na moyo huo huo”. Alisema Mama huyo.
Zuhura Shaban amebahatika kupata mtoto wa kiume anayeitwa Eklam ambaye alizaliwa na matatizo ya utindio wa ubongo na kusababisha kushindwa kukaa, kusimama wala kufanya chochote jambo lililofanya mume wake kumtelekeza yeye na mtoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad