Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi kwa walimu vijana wawili hao wawili ambao wamewapata ufadhili wa masomo kutoka CSI katika Chuo cha Urembo Maznat kilichopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo.
Suzana Kanyara ambaye alipata ufadhili wa Masomo ya Urembo kutoka shirika la Childbirth Survival International(CSI) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna alivyojipanga mara baada ya kupata fursa ya kupata mafunzo ya Chuo cha Urembo Maznat kilichopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo.
David Francis ambaye alipata ufadhili wa Masomo ya Urembo kutoka shirika la Childbirth Survival International(CSI) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kushukuru shirika hilo kwa kumpatia nafasi hiyo ili kujiendeleza kwenye fani ya urembo kupitia Chuo cha Urembo Maznat kilichopo Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo.
Mwalimu wa Chuo cha Urembo Maznat, Juma Kimwaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyowapokea wanafunzi hao na kutoa shukrani kwa shirika la Childbirth Survival International(CSI) kuendelea kuwasaidia vijana ili kufikia malengo yao.
Meneja wa Programu za Vijana katika shirika la Childbirth Survival International(CSI) Ester Mpanda pamoja na wanafunzi wakipata maelekezo kutoka kwa uongozi wa Chuo cha Urembo Maznat mara baaada ya kuwasili chuoni hapo kwa ajili ya kuanza masomo ya urembo.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKA
la Childbirth Survival International(CSI)ambalo imejikita katika
kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua limewashauri
vijana kuhakikisha wanachangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili
kufanikisha ndoto zao kimaisha na kuweza kujitegemea kiuchumi.
CSI
imesema pamoja na mkakati wake wa kuendelea kushirikiana na wadau
wengine ikiwemo Serikali katika kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati
wa kujifungua na wale walio chini ya miaka mitano, bado inao wajibu wa
kuhakikisha ndoto za vijana wa kitanzania zinatimia , hivyo wameamua
kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana wawili katika Chuo cha Urembo cha
Maznat baada ya kuwapata kupitia shindano maalum ambalo lilifanyika mwzi
mmoja uliopita.
Hayo
yamesemwa leo na Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester Mpanda
baada ya kuwakabidhi kwa walimu vijana wawili ambao wamewapatia ufadhili
wa masomo katika Chuo hicho cha Urembo. Akizungumza leo Januri 13,2021
jijini Dar es Salaam Meneja wa Programu za Vijana kutoka CSI Ester
Mpanda amesema wanayo fufaraha kubwa kwani vijana hao wanakwenda
kutimiza ndoto zao za kujitegemea kiuchumi na kimaisha pindi
watakapohitimu masomo yao.
Akifafanua
zaidi Ester Mpanda amesema shirika hilo ambalo limeanzishwa na mama
wawili ambao ni Stella Mpanda anayeishi nchini Tanzania na Tausi
Kagasheki anayeishi Marekani mbali ya kujikita katika kupunguza vifo vya
mama na mtoto, wameona kuna kila sababu sasa ya kuhakikisha linatoa
ufadhili wa masomo kwa vijana wa kitanzania ili waweze kutimiza ndoto
zao ikiwa pamoja na kujiinua kiuchumi baada ya kuhitimu masomo ya urembo
katika chuo hicho.
"Chuo
hiki kinafundisha masuala ya urembo, upambaji, kusuka, kupamba
maharusi, hivyo vijana hawa ambao leo hii wameanza masomo yao hapa baada
ya kuendesha shindano la kutafuta vijana ambao wanatamani kutimiza
ndoto zao kimaisha.
"Tunachoweza
kueleza CSI tumeamua kutoishia kwenye kupunguza vifo vya mama na mtoto,
bali tunayo nafasi ya kujenga maisha ya vijana wa kitanzania ambao
tunatarajiwa wawe baba au mama wa kesho, tunaka kujenga vijana
watakaokuwa baba na mama bora huko baadae ambao watakuwa na uchumi
unaowezesha kuendesha familia zao bila matatizo yoyote,"amesema Mpanda.
Amesisitiza
masomo ambayo vijana hao wameyaanza leo katika chuo hicho yatachukua
muda wa miezi mitatatu na baada ya hapo wataanza kujitegemea katika
safari yao ya kimaisha."Nawashukuru Chuo cha Maznat kwa kukubali kufanya
kazi na sisi na kukubali kutupa nafasi ya kuja hapa na kuwaleta vijana
hawa ambao kwa upande wetu tutagharamia kila kitu kinachohusu masomo yao
kwa muda wote.
"Ninachoweza
kuwaambia vijana mkisikia fursa tunaomba mzichangamkie kwani huwezi
jua,hawa vijana ambao wanaanza masomo leo walikuja tu kwenye shindano
letu na wala hawakujua kama watashinda lakini walipata nafasi na leo
wako hapa..Nafasi ziko nyingi hivyo ni jukumu la vijana kuzitafuta
kokote ziliko."
Kuhusu
changamoto ya kuchagua kazi, Mpanda amesema ni kweli kuna baadhi ya
vijana wamekuwa na utamaduni wa kuchagua kazi, jambo linalochangia
kuwakwamisha kimaendeleo, hivyo ni vema wakabadilika.
"Kwa
sasa kuna utofauti kidogo vijana wamebadilika wameanza kushughulika
katika kazi mbalimbali maana wameona hali ilivyo na wamekubali matokeo,
wanafanya kazi yoyote ilimradi iwe ya halali na isiyovunja sheria."
Kwa
upande wake mmoja ya walimu katika Chuo cha Urembo Maznat Juma Kimwaga
amesema wamefurahi kuwapokea wanafunzi hao wawili akiwemo wa kijana wa
kiume."Viajana wengi wa kiume huwa wanachagua kazi na hasa hizi za
urembo lakini ukweli kazi ya urembo ina fursa ila hawajui hilo.
"Tunawapongeza
CSI kwa uamuzi huu mzuri wa kufanikisha ndoto za vijana hao kwa
kuwaleta katika chuo chetu, tunaamini wakitoka hapa watakwenda
kujitegemea kimaisha,"amesema.
Aidha
amesema katika fani ya urembo, kuna changamoto kubwa ya kupata wanaume
wakiamini sio kazi ambayo wanastahili kuifanya, hivyo kupata kijana wa
kiume kwani ni jambo la kujivunia."Vijana hawana sababu ya kuigopa
tasnia hii ya urembo, sisi tuko huku maisha yanakwenda na maendeleo
tunafanya kwa kiwango kikubwa tu."
Kwa
upande wa vijana hao ambao ni Susan Kanyara na David Frank wamesema
wanashukuru kwa kupata fursa hiyo ya kudhaminiwa na CSI kusoma chuoni
hapo.Waliipata nafasi hiyo baada ya kushinda shindano la CSI
lililofanyika mwezi mmoja uliopita.
Susan
Kanyara amesema leo wameanza masomo katika chuo hicho na ni matumaini
yake anakwenda kutimiza ndoto zake za kimaisha na hasa kujitegemea.
Wakati
David Francis amesema nafasi hiyo aliyoipata ni ya kipekee, hivyo
atasoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zake huku akitoa shukrani kwa CSI
kwa hatua ambayo wameichukua ya kusaidia vijana walioko mtaani kutimiza
ndoto zao kupitia ufadhili huo wa masomo.
No comments:
Post a Comment