HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 13, 2021

WAKAGUZI WA NGOZI WATAKIWA KUSIMAMIA UZALISHAJI WA NGOZI BORA

 


Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo, Usalama wa Chakula na Lishe, Bw Gabriel Bura amewataka wakaguzi wa zao la Ngozi wa Kanda ya Mashariki kusimamia ubora wa Ngozi zinazozalishwa.

Bura ameyasema hayo leo (12.01.2021) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya wakaguzi wa Ngozi wa Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Pwani na Morogoro) yanayofanyika katika ukumbi wa Mvuvi House jijini Dar es Salaam.

Wakaguzi hao wa Ngozi wametakiwa kusimamia uzalishaji wa zao hilo katika hatua zake zote ili kupata Ngozi zinazofaa kusindikwa katika viwanda. 

Aidha, wakaguzi hao wametakiwa kutumia sheria namba 18 ya mwaka 2008 inayolenga kuboresha zao la ngozi ili wadau waweze kuzalisha ngozi bora inayokidhi mahitaji ya viwanda vyetu na hatimaye kuwa na tija ya uzalishaji wa zao hilo.

Bura amesema uzalishaji wa ngozi za ng’ombe na mbuzi kwa siku ni vipande 31,000 lakini ni asilimia 10 tu ya ngozi zinazopelekwa viwandani hufaa kwa ajili ya kusindikwa, na asilimia 90 hazifai kutokana na kukosa ubora unaofaa kwa ajili ya kusindikwa.

“Hivyo baada ya kupata mafunzo haya ni matarajio ya wizara kuwa mtakwenda kulisimamia nyema zao hili la Ngozi ili kuhakikisha Ngozi yote inayozalishwa inakuwa bora,” alisema Bura.

Hapa nchini vipo viwanda viwili tu vyenye uwezo wa kusindika ngozi hadi hatu ya mwisho ambavyo ni Moshi Leather Industry chenye uwezo wa kusindika futi za Mraba elfu 15,000 kwa siku na Himo Tannery and Planter Ltd chenye uwezo wa kusindika futi za mraba 10,000 kwa siku. 

Uwezo wa usindikaji wa viwanda vyote viwili kwa siku ni sawa na vipande 1000 vya ngozi ya ng’ombe na 9000 vya ngozi ya mbuzi, hivyo bado kuna uhitaji wa viwanda vya kusindika Ngozi na vilivyopo kuongeza uwezo wake wa kusindika zao hilo.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo,Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya Mifugo) Bw.Gabriel Bura akizungumza na wakaguzi wa Ngozi  Kanda ya Mashariki  wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo,Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya Mifugo) Bw.Gabriel Bura akiwa katika picha ya Pamoja na wakaguzi  wa Ngozi Kanda ya Mashariki mara baada ya kufunguliwa mkutano huo.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad