HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 12, 2021

Ruzuku kutoka COSTECH yaiwezesha TALIRI Tanga kupima uzito wa ng'ombe kidijitali

KITUO cha Utafiti wa Mifugo Tanga kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) kilianzishwa miaka ya 1950 kikiwa na jukumu la kufanya utafiti wa malisho ya mifugo katika Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

Taasisi hii ni kongwe na imekuwa na changamoto ya uchakavu wa majengo pamoja na miundombinu ya kufanya utafiti hivyo kupelekea kuwepo kwa uhitaji wa ukarabati na ujenzi wa majengo mapya ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, kutokana na mahitaji hayo kituo kiliomba Ruzuku kutoka Serikalini kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili kufanya maboresho ya maabara, jengo la kufundishia kwa vitendo ufugaji kuku wa kisasa, chumba cha kupozea pamoja na mizani ya kisasa ya kidijitali ya wanyama.

Ufungaji wa mizani ya kidijitali upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji, mfumo huu utakapokamilika utawezesha kutambua uzito wa mfugo ambao ni muhimu sana kwa kila mfugaji, daktari wa mifugo hata watafiti. Kipimo hiki husaidia kutambua maendeleo ya afya ya mfugo husika, kuandaa chakula kinachoendana nayo, kukadilia dozi ya dawa pindi mfugo ukiugua hata kukadilia kiwango cha mazoezi anayohitaji kwa ajili ya uzalishaji wenye tija.

Ruzuku iliyotelewa na Serikali kupitia COSTECH imesaidia taasisi hiyo katika utekelezaji wa miradi hivyo kwani imekiwezesha kituo kudhibiti ubora wa mazao ya mifugo na malisho kwa mikoa ya kanda ya pwani.

Mradi huu unaojumuisha miundombinu mitatu ni muhimu kwa kwa unaleta tija kwa wadau wa sekta ya mifugo kuanzia taasisi yenyewe, wafanyakazi wake, wakulima, wazalishaji na waagizaji wa chanjo.
Muonekano wa jengo la maabara katika kituo cha Utafiti wa malisho ya Mifugo TALIRI-Tanga ambalo limejengwa kwa ruzuku kuutoka Serikalini kupitia COSTECH
Banda linalotumiwa na kituo cha TALIRI Tanga kwenye utafiti wa kuku.

Mzani wa kisasa wa kidijitaliunaotumika kupima uzito wa wanyama katika Kituo cha Utafiti TALIRI-Tanga ambao umejengwa kwa ruzuku kutoka Serikalini kupitia COSTECH

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad