Naibu
Waziri Kilimo Hussein Bashe akiwa amebeba dumu la lita 5 la mafuta ya
alizeti alilopewa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka baada ya
kutembelea kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti cha Bugali Investment
Ltd cha mkoani Simiyu mara baada ya Naibu Waziri Bashe kutembelea
kiwanda hicho cha kukamua mafuta ya alizeti kwa kiwango cha hali ya juu
(Double refined).
NAIBU
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (Jana) tarehe 17 Januari, 2021 amewasili
mkoa wa Simiyu kwa ajili ya tukio la tukio la kihistoria la utiaji
saini mkataba wa kuongeza tija na uzalishaji katika zao la pamba kati ya
Bodi ya Pamba, Vyama vya Ushirika na Vyama vya Msingi vya Mazao (AMCOS)
na Tume ya Maendeleo ya Ushirika na kuwahamasisha Viongozi wa mkoa wa
Simiyu kuanzisha mashamba makubwa (Block Farming) ya kilimo cha alizeti.
Waziri
Bashe amesema Wizara ya Kilimo imedhamiria kutekeleza kauli ya Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
aliyoitoa wakati akizindua Bunge la 13 na kusisitiza umuhimu wa kuitumia
Sekta ya Kilimo mazao kuleta maendeleo ya kweli kwa Watanzania na
kuwafanya Watanzania kuwa mabilionea.
Waziri
Bashe amewaaambia Viongozi wa mkoa wa Simiyu kuwa ili mkoa uwe na
uwekezaji unaolipa ni lazima kufikiria kutumia uzalishaji wa mazao ya
kilimo kwa njia ya uwekezaji katika mashamba makubwa (Block Farming)
ambapo Naibu Waziri Bashe ameahidi Wizara itatoa Wataalam kuanzia kwenye
kufanya uchunguzi wa udongo kabla ya kuanza kwa uzalishaji na baadae
utaalam katika kilimo cha zao la alizeti.
Waziri
Bashe amesema mkoa wa Simiyu utapaa kimapato kutokana na uanzishwaji wa
mashamba makubwa (Block Farming) kwa kuwa ni rahisi kuendesha mashamba
makubwa ambapo ni rahisi kuwasaidia Wakulima wakiwa katika eneo moja
lakini pia ni rahisi kutoa utaalam na ushauri wa kuandaa mashamba,
utoaji wa pembejeo bora, usimamizi.
“Ni rahisi kuwapa mikopo na teknolojia za kilimo na uvunaji kwa Wakulima walio pamoja kuliko walio mbali.”
“Ni
rahisi kutumia teknolojia za uvunaji pamoja na uhifadhi lakini pia kazi
uwa ni rahisi kwa mnunuzi anapotaka kununua mzigo na kuuchukua kutoka
kwa Wakulima walio katika eneo moja.”
“Naomba
pia niwaeleze ni rahisi pia Halmashauri zenu kukusanya tozo na ushuru
mbalimbali kwa Wakulima walio kwenye shamba la pamoja.” Amekaririwa
Naibu Waziri Bashe.
Waziri
Bashe ameongeza kuwa Sekta ya Kilimo mazao hususan kilimo cha alizeti;
Ikitumika ipasavyo mkoa wa Simiyu unaweza kuongeza mapato ukilinganisha
na Sekta nyingine za kiuchumia.
“Napenda
niwakikishie kuwa soko la alizeti lipo wazi na mnafahamu kuwa Serikali
inatumia zaidi ya Bilioni 443 kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi”.
Amesisitiza Waziri Bashe.
No comments:
Post a Comment