MGOGORO WA SHAMBA MBOPO WATUA KWA DIWANI MABWEPANDE, UAMUZI KUTOLEWA JUMATATU IJAYO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 27, 2021

MGOGORO WA SHAMBA MBOPO WATUA KWA DIWANI MABWEPANDE, UAMUZI KUTOLEWA JUMATATU IJAYO

 

Diwani wa Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam,Muhajirina Kassim  akizungumza na Michuzi Tv leo baada ya kikao cha kutafuta uhalali wa eneo la shamba linagombaniwa kwa muda mrefu kati ya wananchi wa Mbopo na mmoja ya watu anayedaiwa kuwa ndio mmiliki wa shamba hilo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo kata ya Mabwepande   wilaya ya Kinondini jijini Dar es Salaam,Mohamed Bushir akifafanua jambo baada ya kikao hicho. 
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
VIONGOZI wa Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwemo Diwani wa Kata hiyo Muhajirina Kassim wameendelea kufanya vikao kwa lengo la kutafuta uhalali wa eneo la shamba linagombaniwa kwa muda mrefu kati ya wananchi wa Mbopo na mmoja ya watu anayedaiwa kuwa ndio mmiliki wa shamba hilo Emmanuel Mgalaa

Katika kutafuta ufumbuzi huo , viongozi hao wakiongozwa na Diwani huyo aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho kilichokutanisha pande zote mbili ikiwemo ya wawakilishi wa wananchi wa Mbopo ,Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo Mohamed Bushir pamoja na Mgala walikutana na kufanya mazungumzo.

Akizungumza kuhusu kikao hicho ambacho kinalengo la kufata ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo ili kuhakikisha amani na usalama unaendelea kutawala, Diwani wa Kata ya Mabwepande Muhajirina Kassim ameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kikao cha kwanza kimekwenda vizuri na kimetoa muelekeo unaokwenda kumaliza mgogoro huo.

Amesema baada ya pande zote kusikiliza pande zote mbili wamefikia makubaliano kwamba Jumatatu ya wiki inayokuja wakutane tena ili kutoa uamuzi wa nani mmiliki halali wa shamba hilo ambalo linagombaniwa kwa wananchi wa Mbopo kueleza ni la kwao na wakati huo huo Mgala naye kudai ni la kwake.

"Leo tumekutana katika kikao kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa shamba hilo ambalo lipo eneo la Mbopo , kumuwepo na mgogoro wa muda sasa, wananchi wanasema ni eneo lao na wakati huo huo Emmanuel Mgala naye anasema ni la kwake.Katika mazungumzo yetu wananchi wamethibitisha eneo hilo ni lao kwa maneno kwani hawakuwa na nyaraka, na Mgala naye amethibitisha kwa maneno na kuonesha nyaraka alizonazo.

"Hivyo tumeamua Jumatatu ya wiki ijayo tutakutana tena hapa Ofisi za Mtendaji Mabwepande kuanzia saa Nane mchana, kila upande uje na vilelezo vya nyaraka zote muhimu, mashahidi wote ambao watatoa maelezo ya kina kuhusu ukweli wa shamba hili.Mimi ni Diwani wa Kata ya Mabwepande , nimechaguliwa na wananchi ili kuhakikisha nashirikiana nao katika kuleta maendeleo ya Kata yetu, pia kwa nafasi yangu mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kata, hivyo lazima nitafute ufumbuzi wa jambo hili, na baada ya hapo tuendelee na shughuli za kuleta maendeleo,"amesema Kassim.

Amesisitiza atahakikisha anasimama kwenye haki, katika kuamua kuhusu nani mmiliki halali wa shamba hilo, hataki kuwa sehemu ya kufanya dhuluma."Ikiwa eneo hili ni la wananchi basi nitawapa, ikiwa vilelezo vya Mgala navyo vitathibitisha ni eneo kupitia kikao hicho basi atapewa eneo lake."

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbopo Hassan Bushir ambaye alishiriki kwenye kikao hicho kama mmoja ya wajumbe, ameeleza kikao kimekwenda vizuri kwa pande zote kusikilizwa lakini wamefikia muafaka Jumatatu watakutana tena kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

"Nimeshiriki katika kikao hiki kilichoitishwa na Diwani wetu kama Mjumbe tu na sio Mwenyekiti wa Serikali ya Mbopo, lakini nachoweza kueleza, kikao kimekwenda vizuri, tunasubiri hiyo Jumatatu tutakapokutana tutapa muafaka.Binafsi natamani kuona mgogoro huu unafika mwisho,"amesema Bushir.

Wakati huo huo Emmanuel Mgala amezungumzia kikao hicho ambapo ameweka wazi anasubiri hiyo Jumatatu ili aoneshe vielelezo alivyonavyo kuhusu umiliki wake katika shamba hilo."Shamba lile ambalo lipo Mbopo ninamiliki kihalali, nyaraka zote ninazo nitazileta hiyo Jumatatu kwenye kikao.

"Ingawa na leo hizo nyaraka nimezionesha pale kikaoni, nitakuja na mashahidi wote na bahati nzuri aliyeniuzia naye yupo na siku hiyo atakuwepo kutoa ushahdi wake.Baada ya hapo tutasubiri maamuzi ya kikao ambayo yatatolewa baada ya pande zote kusikilizwa,"amesema Mgala.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad