HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 13, 2021

MGANGA MKUU PWANI AWAONYA WANAFUNZI KUACHANA NA TABIA YA KUJISAIDIA VICHAKANI

 

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dk. Gunini Kamba akizungumza jambo katika moja ya mkutano na wadau mbali mbali wa sekta ya afya kwa ajili ya kujadili masuala mbali mbali yanayohusiana na utoaji wa huduma za afya.

……………………………………………………………………………………….

NA VICTOR MASANGU  , PWANI

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Gunini Kamba amewawatahadharisha na kuwaonya vikali  baadhi ya  wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari  kuachana kabisa na vitendo vya kujisaidia  katika maeno ya vichake kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha madhara makubwa ya  kutokea kwa mlipuko wa magonjwa mbali mbali ikiwemo kipindu pindu.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na   mikakati waliyojiwekea katika ngazi ya Mkoa katika kupambana na kudhibiti katiba hali ya kuwepo kwa magonjwa ya mlupiko katika maeneo mbali mbali hususana katika mkusanyiko wa wtu wengine kama vile mashuleni.

“Kwa sasa hivi tupo katika msimu mpya wa mwaka wa 2021 ambapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari tayari wamefungua shule zao na kuanza masomo lakini pamoja na mambo mengine yote ni lazima sisi kama wataalamu wa afya tuweke mipango madhubuti ya kuwalinda watoto wetu hasa katika kipindi hiki na kuwatahadharisha na kutojisaidia ovyo ovyo katika maeneo ya vichaakni kwani hii ni hatari sana kupata magonjwa ya mlipuko.

Aidha Kamba alifafanya kubwa kwa kipindi hiki cha ni lazima viongozi wa shule pamoja na mamlaka zinazohusika kuhakikisha kwamba wanazingatia maagizo ambayo yanatolewa na wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuweka mafi safi na salama katika maeneo ya shule ili wanafunzi wanapotoka kujisaidia waweze kusafisha na kunawa mikono yao kwa lengo la kuthibiti milipuko ya magonjwa hayo.

Pia aliongeza kuwa katika kupambana na wimbi la mlipuko wa magonjwa wanaendelea kushirikiana bega kwa bega na walimu wa shule mbali mbali zilizopo katika Mkoa wa Pwani juu ya kuwaelimisha umuhimu  wa usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi na kuwapa mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia katika kuwaelimisha watoto wao katika kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na uchafu.

“Suala la baadhi ya wanafunzi au jamii yoyote kuwa na tabia ya kujisaidia katika maeneo ya vichakani hii sio sahii kabisa hata kidogo kwani ni hatari zaidi kutokea kwa magonjwa ya milipuko kama vile kuumwa na tumbo,kuhara na  kuibuka kwa  ugonwa wa kipindipindu na kitu kingine mtu anaweza kujisaidia na mvuaikaja kunyesha hivyo ikikisomba kinyesi kunaweza kuleta madhra makubwa katika jamii ambayo ipo karibu na maeneo hayo.

Katika hatua nyingine Kamba aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya afya na kuwapatia huduma ya matibabu wananchi wake hivyo isingependa kuona hali ya kuwepo kwa magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kuthibitiwa endapo jamii ikizingatia kanuni na taratibu zote  ambazo zinatolewa na watalaamu wa sekta ya afya ili kuondokana kabisa na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad