IDADI YA WATU 800 WAKABILIWA NA MATATIZO YA UTAPIA MLO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 26, 2021

IDADI YA WATU 800 WAKABILIWA NA MATATIZO YA UTAPIA MLO

  Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -Arusha

KUFUATANA na takwimu za Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) limebaini kuwa takribani watu milioni 821 wanakabiliwa na matatizo ya utapiamlo yanayotokana na kula vyakula visichokuwa na viini lishe bora.

Hayo yalibainishwa na waziri Mkuu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa shirika la agri thamani  foundation Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa kimataifa  unaoangazia mazao ya kiasili  ya afrika  inayofanyika mkoani hapa Katika ukumbi wa hotel ya gran melia ambapo alisema kuwa kuwa upande wa hapa nchini Tanzania Hali ya utapiamlo ni mbaya  kulingana na takwimu za utafiti wa hali lishe  ya mwaka 2018 ambazo zinaonyesha watoto wengi ndio wanaathieriwa sana na tatizo hilo.

Alisema kuwa kulingana na takwimu hizo zinaonyesha watoto wenye umri kuanzia miaka 0 - 5 milioni tatu  wamedumaa,watoto wa miaka 0-5  milioni 1.3 wanauzito pungufu, watoto wenye umri wa miaka 0-5  milioni tano wanaupungufu wa Damu,, watoto wenye umri huohuo 0-5 milioni tatu wanaupungufu wa vitamin A na asilimia 32 ya wanawake wenye umri wa miaka 14 -49 wanatatizo la uzito uliozidi.

Alibainisha baadhi ya adhari ya utapia mlo ni pamoja na udumavu ambao una athari Katika makuzi na maendeleo ya watoto kwa sababu hupunguza ufahamu na ubunifu kati ya asilimia 30 hadi 40 ambapo hali hiyo huadhiri uwezo wa mtoto kufundishika ,kuelekezwa na kushusha ufaulu, na pia utapia mlo unaongeza magonjwa na vifo vya watoto na akina mama.

"Miongoni mwa asilimia 50 ya magonjwa ambayo husababisha vifo vya watoto wenye umri Chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na utapiamlo ,pia wanawake takribani 60,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya upungufu wa damu yanayotokana na tatizo la upungufu wa damu linatokana na upungufu wa madini china.

Aidha alisema kuwa mazao ya mboga ni muhimu kwenye afya lishe kwani utafiti wa kitaalam unaonyesha kuwa mboga za asili ya afrika  zina viwango vikubwa vya viini lishe ukilinganisha na mboga zingine kutoka mataifa ya nje ya bara la Africa ambapo alibainisha kuwa watu wa nje ya afrika wanayaita mazao haya kuwa ni “super foods”  yaani vyakula venye viini lishe bora kabisa.

"Afrika tunazaidi ya aina 400 za mazao ya mboga za kiasili lakini yale yanayotumika Kama chakula ni machache Sana na yale yanayotumika kibiashara ni machache zaidi ,huu ni urithi wetu wa mazao haya nilazima tuyatunze na kuyaenzi kwa sababu mbalimbali moja wapo ikiwa mazao ya mboga  ni muhimu Sana kwa afya lishe ,pia kwa ajili ya kutunza bioanuai yetu isipotee

Alisema mbali na mazao ya mboga kusaidia kupunguza utapia mlo pia ni fursa kubwa Sana ya kibiashara Katika ngazi ya kaya na taifa kwa ujumla ,kwa  afrika na Tanzania ambapo ukienda sokoni utaona kuwa mboga hizi zimekuwa njia moja wapo ya kujipatia kipato hasa kwa kina mama na vijana .

"Tanzania Kutambua ukubwa wa tatizo hili imeamua  kupitia ilani ya uchaguzi ya chama tawala CCM 2020-2025 kuweka uzito mkubwa kwa kuahidi  kuhamasisha kilimo cha mazao lishe Ili kupunguza udumavu kutoka Asilimia 32 hadi 24,pamoja na kupunguza ukondefu Ili kuendelea kuwa chini ya Asilimia 5 kiwango ambavyo kimewekwa na dunia, pia kuongeza uzalishaji wa mazao ya bustani kutoka Tani 7,230,217 hadi tani 14,600,000ifikapo mwaka 2025 na Ili kufikia malengo haya tuneainisha mambo kadhaa ikiwemo kujengea uwezo wa taasisi za ndani za serikali na binafsi za ithibati Ili kupunguza gharama za ithibati za mazao yanayosafirishwa nje hasa mazao ya bustani na mboga ambavyo wawekezaji wake wakuu ni wanawake na vijana "alibainisha Pinda

Pinda alisema kuwa kazi ya kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya mazao ya mboga yenye asili ya kiafrika si kazi ya serikali tu bali ni kazi ya wadau wote wakiwemo ,watafiti ,wakulima,wafanyabiashara na sekta ya usafirishaji,uuzaji wa mazao  ghafi na usindikaji  wote wakiungana watafanya kazi nzuri ,aidha alitoa wito kwa wadau wa Maendeleo wa sekta binafsi na ile ya serikali kufanya Kila linalowezekana Kuhakikisha mazao haya yanapewa kipaumbele,pia niasisitize ni vyema tukaweka nguvu nyingi katika utafiti na hasa Katika maeneo ya ukusanyaji ,utunzaji na uboreshaji wa mbegu za mazao haya ulimaji bora na matumizi yenye kuimarisha lishe na afya ya mlaji

Naye mkurugenzi wa kanda ya mashariki na kusini mwa afrika ,world vegetable center Dkt.Gabriel Rugalema alisema kuwa mkutano huo utasaidia kuhakikisha wanajenga mkakati utakao hamasisha ongezeko la mazao haya pamoja na namna ya kuyatunza 

Alisema kuwa zaidi ya watu 200 wameshiriki moja kwa moja mkutano huu na watu mengine 1000 wameshiriki kwa njia ya mtandao hiyo inatokana na kuwepo na mlipuko wa Mara yapili ya ugonjwa wa Covid 19.

Naye mchumi wa baraza la biashara la afrika mashariki (EABC)  Adrian Njau aliwataka watu  wajikite kwenye mazao yetu wenyewe kuliko kutegemea  mazao  ambayo yanatoka nje ,huku akiwasisitiza wataalam waendelee  kufanya utafiti zaidi wa mboga za ndani.
Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Agri Thamani Foundation Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari Jana Mara baada ya kufungua mkutano wa duniani wa kujadiliana jinsi ya kuhamasisha na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika inayofanyika jijini hapa  ambapo aliwasisitiza wanahabari kutumia kalama zao kuelimisha wananchi namna ya kupambana na tatizo la utapia mlo kupitia kilimo cha mboga na matunda.
mtafiti wa mazao ya mboga kutoka kituo Cha kimataifa cha utafiti wa mazao ya mboga ya asili ya kiafrika (world vegetable center ) Inviolate Dominick    akitoa maelekezo ya umuhimu wa viungo kwa ajili ya kuboresha lishe,afya ,na hata kibiashara  kwa mmoja ya mshiriki wa mkutano wa duniani wa kujadiliana jinsi ya kuhamasisha na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika inayofanyika jijini hapa.
(Picha na Woinde Shizza , ARUSHA)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad