HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 10, 2020

WAZIRI AWESO ATAKA KAZI ZIFANYIKE KWA WELEDI

 

 

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma. (Hawapo Pichani)

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi David Palangyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa kikao kilichoongozwa na Waziri wa Maji  Mhe. Jumaa Aweso. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga.

***********************************

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewataka wataalam katika sekta ya maji kuzingatia weledi katika utendaji.

Waziri Aweso amesema hayo katika kikao chake na watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), ambapo amesisitiza ipo haja ya kuimarisha huduma ya upatikanaji maji katika jiji la Dodoma.

Waziri amewapongeza DUWASA kwa kazi wanayoifanya na kuwataka kuongeza nguvu zaidi katika huduma kwa wateja na kuhakikisha huduma inawafikia wakazi wa Jiji la Dodoma kama inavyostahili katika maeneo yote.

“Tunahitaji kufanya kazi kwa kasi kubwa ili kuboresha huduma ya maji katika jiji la Dodoma, hivyo tuongeze nguvu ya utendaji kazi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea,”  Waziri Aweso amesema na kuongeza  kuwa lazima watumishi watumie taaluma na weledi wa fani zao kwa kushirikiana ili kuhakikisha huduma ya maji inaimarika zaidi.

Waziri Mhe. Aweso amezitaka taasisi zote zilizopo chini ya Wizara ya Maji kuchukua hatua ili kuimarisha huduma ya upatikanaji maji nchini na kufanya kazi kwa kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali ili wananchi wapate huduma ya maji iliyo bora.

Wakati huohuo, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemtaka Katibu Mkuu, Mhandisi Anthony Sanga kumbadilisha kituo cha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi David Palangyo.

Kikao hicho kilichowakutanisha watumishi wa DUWASA, kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Mhandisi Anthony Sanga pamoja na Naibu Katibu Mkuu Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad