NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MKOA
wa Pwani ,umepiga hatua kali na kufikia kuwa na viwanda vikubwa,vya
kati,vidogo na vidogodogo 1,236 kwa mwaka 2020 kutoka viwanda 396 kwa
mwaka 2016.
Kasi hiyo ya
ujenzi wa viwanda ni kubwa ndani ya miaka minne ,ambapo viongozi
watendaji wa mkoa huo wameamua kuongeza jitihada za kuhamasisha
wawekezaji ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa UKANDA WA VIWANDA.
Akielezea
mafanikio hayo ,mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema
,bado wamejipanga kuongeza viwanda na wawekezaji ili kutekeleza ilani
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pamoja
na hayo ,alieleza kati ya wilaya zote mkoani hapo ,lakini bado wilaya
tatu ya Kibiti,Rufiji na Mafia zinasuasua kufikia kasi hiyo .
Kutokana na hilo ,ameelekeza nguvu ielekezwe katika wilaya hizo kwani fursa zipo .
"Tunapokea
pongezi na sifa nyingi kutoka kwa viongozi wakuu Taifa akiwemo Rais
John Magufuli ,mikoani na nchi mbalimbali hivyo nawataka viongozi mkoa
kuendelea kulinda maendeleo hayo na kuinua sekta ya viwanda" alibainisha
Ndikilo.
Akielezea juu
ya sekta ya elimu ,ameelekeza kuhakikisha madarasa yanayopaswa kujengwa
yajengwe ,ili wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
January 2021 wawe wote darasani ,kwani bado wanafunzi 6,577 wanaonekana
watakosa kuingia madarasani.
Akizungumzia tatizo la upungufu wa watumishi , alisema pamoja na juhudi za mkoa lakini changamoto hii inajirudia kila mwaka.
Katibu
tawala msaidizi mipango na uratibu Edward Mwakipesile alifafanua ,kuna
changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi mbalimbali na idara ya afya
upande wa wataalamu wa Xray ni shida .
Nae mkuu wa wilaya wa Mafia , Shaibu Nnduma alisema ,idara 14 zinakaimisha watendaji na wote wanaokaimu hawana sifa.
Kufuatia
changamoto hiyo ,katibu mkuu TAMISEMI alifikishiwa taarifa hizo na
kuomba tena awasilishiwe juu ya hilo na kuhusiana na tatizo la Mafia
amedai atafika mwenyewe Mafia .
No comments:
Post a Comment