EQUITY Tanzania leo imezindua nembo mpya ya utambuzi unaoendana na safari ya mabadiliko inayoendelea ndani ya kampuni mama ya Equity Group Holdings. Uzinduzi huo mpya unalenga kuiweka kampuni katika njia ya ukuaji endelevu na utoaji huduma bora zinazoendana na mabadiliko yanaoendelea katika mazingira ya sekta ya fedha.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Serena Hoteli jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti alisema
kuanzia sasa, Equity Tanzania itajitambulisha kwa nembo iliyobeba kikapu
kilichosheheni bidhaa na huduma mbali mbali zakifedha chini ya paa
moja.
Alisema
nembo mpya sasa itaonyesha “Equity” bila neno Benki kama ilivyozoeleka
ili kuonyesha dhamira ya kampuni ya kuwa kituo cha kutoa huduma mbali
mbali jumuishi zakifedha ndani ya paa moja, huku ikiambatana na ahadi ya
usimamizi imara wa uhusiano, uwezeshaji wa wateja binafsi na biashara.
“Muonekano
wetu mpya unaleta uhakika wa uwezeshaji wa watu binafsi ili kupanua
fursa zao katika kuleta utajiri. Tutazindua muonekano mpya katika matawi
yetu yote, njia zetu za kutolea huduma zakibenki kidijitali, mitandao
yakijamii, tovuti, njia zakibenki kupitia simu za kiganjani, biashara
mtandaoni na mashine za kutolea fedha. Kuanzia sasa mtaanza kuona alama
za nembo yetu mpya katika matawi yetu ikiwa ni sehemu ya programu yetu
ya mabadiliko,” alisema Kiboti.
Aidha
aliongeza kuwa wateja kwa sasa watarajie kupata huduma bora kabisa bila
kuwepo na aina yeyote ya hitilafu wakati benki ikijipanga kukuza idadi
ya wateja wake.
“Tutaendela
kubuni huduma bora kwa lengo la kupanua upatikanaji wa huduma jumuishi
zakifedha nchini kote…Tutaimarisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa
njia ya simu za kiganjani na kupeleka huduma zetu mpaka maili ya mwisho
kupitia Equity Wakala. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Mawakala wetu
wanaendelea kujipatia pato la ziada na kutengeneza ajira mijini na
vijijini. Tunaahidi kuendelea kuwa wabunifu na wenye umuhimu wakati
ambapo mahitaji ya wateja wetu yanabadilika kulingana na malengo na
ndoto zao,” alisema Kiboti.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond
Mbilinyi akitoa historia ya benki hiyo nchini alisema, ilianza kufanya
biashara mnamo Februari 2012 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), huku ikiendelea kufanya vizuri kibiashara na pia ni
mjumbe wa Taasisi inayosimamia taaluma ya kibenki nchini, Tanzania
Institute of Bankers.
"...Ikiwa
na Makao Makuu yake Dar es Salaam, Benki ya Equity Tanzania inayo jumla
ya matawi 14 huku pia huduma zake zikipatikana kwa Mawakala wapatao
3,634, jumla ya sehemu za kutolea huduma 4,410 pamoja na Mashine za
Kutolea Fedha 21. Benki ya Equity Tanzania ni kampuni tanzu ya Equity
Group Holdings Plc, ambayo imeorodhesha katika masoko ya hisa ya Nairobi
(Kenya), Uganda na Rwanda," alisema Eng. Mbilinyi.
Alibainisha
kuwa Equity Group Holdings Plc pia hutoa huduma zakibenki katika nchi
za Kenya, Sudani Kusini, Rwanda, Uganda, Tanzania na DRC. Equity Group
Holdings Plc pia inayo ofisi ya biashara nchini Ethiopia. Alisema tangu
Equity ianze huduma nchini Tanzania 2012, imekuwa ikilenga kubadilisha
maisha, kujenga heshima na kupanua fursa za kutengeneza utajiri.
"Kwa
kushirikiana na washirika wetu kibiashara, wateja na wadau wetu wa
kimkakati, tumeweza kupata habari nyingi nzuri kutoka kwa watu mbali
mbali na biashara zikielezea ni jinsi gani walivyonufaika na huduma
zetu. Safari hii ya kubadilisha maisha pia imeshuhudia biashara yetu
nayo ikibadilika. Tumepanua na kubadilisha mtindo wetu wa biashara kwa
kiasi kikubwa sana huku tukiendelea na utamaduni wetu wa kujibadilisha
na kuwa wabunifu zaidi katika kuwahudumia wateja wetu kupitia matawi na
njia zakidijitali."
Alibainisha
kuwa, wateja wao hawalazimiki kutembea kutoka tawi moja kwenda nyingine
au kutoka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine kwani wataweza
kupata huduma zote zakifedha wazitakazo kwa yeyote yule aliyebeba nembo
ya Equity, jambo ambalo alijinasibu kufanikiwa huku kazi hiyo
ikiendelea. Kwa pekee aliwashukuru kwa ushirikiano wote wanaoutoa na
kuahidi kuendelea kuwa pamoja wakati wa utekelezaji wa azma yenye
ujasiri mwingi katika uwepo wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti pamoja na Mwenyekiti wa Bodi
ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi wakizindua nembo yao mpya ya
Equity Tanzania mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa
Habari,leo jijini Dar.
Pichani
kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania Robert Kiboti na
Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Eng. Raymond Mbilinyi
wakipongezana mara baada ya hafla fupi ya uzinduzi wa nembo yao mpya ya
Equity Tanzania mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari
(hawapo pichani),leo jijini Dar.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti kwa pamoja na Mwenyekiti wa
Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi wakizindua nembo yao
mpya ya Equity Tanzania mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa
Habari,leo jijini Dar.Pichani kulia ni nembo iliyokuwa ikitumika hapo
awali
Mkurugenzi
Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti akizungumza mbele ya Wageni
waalikwa wakiwemo Waandishi wa Habari leo jijini Dar,wakati wa uzinduzi
wa nembo yao mpya inayoendana na safari ya mabadiliko.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi akieleza historia
ya benki hiyo nchini mbele ya Wageni waalikwa wakiwemo Waandishi wa
Habari leo jijini Dar,wakati wa uzinduzi wa nembo yao mpya. Mhandisi
Mbililinyi alisema benki hiyo ilianza kufanya biashara mnamo Februari
2012 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), huku
ikiendelea kufanya vizuri kibiashara na kwamba benki hiyo ni mjumbe wa
Taasisi inayosimamia taaluma ya kibenki nchini, Tanzania Institute of
Bankers.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa EQUITY Tanzania pamoja na Wadau wengine wakifuatiliia
kwa makini uzinduzi wa nembo mpya ya utambuzi unaoendana na safari ya
mabadiliko inayoendelea ndani ya kampuni mama ya Equity Group Holdings.
Uzinduzi huo mpya umelenga kuiweka kampuni hiyo katika njia ya ukuaji
endelevu na utoaji huduma bora zinazoendana na mabadiliko yanaoendelea
katika mazingira ya sekta ya fedha.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Equity Tanzania ,Ester Kitoka akiwashukuru Wageni
waalikwa balimbali wakiwemo Waandishi wa Habari waliofika kwenye tukio
la uzinduzi wa nembo mpya wa
Sehemu ya viongozi Waandaminizi wa Equity Tanzania wakifuatilia kwa makini wakati wa uzindzuzi wa nembo mpya wa kampuni hiyo
Sehemu
ya Meza kuu ikishuhudia mabadiliko ya nembo mpya ya Equity
Tanzania,hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa
na Wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari
No comments:
Post a Comment