HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 3, 2020

WAZAZI CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI

 


Na Woinde Shizza, ARUSHA

WASICHANA wa shule ya Sekondari Enyoito, wamelalamikia umaskini na wazazi kutokuwafuatilia watoto wao ndio chanzo cha mimba za utotoni.

Wamesema hayo wakati wa mdahalo wa namna ya kukabiliana na changamoto za ujana, zinazopelekea wasichana kupata mimba, mdahalo uliofanyika kwenye ukumbi mdogo, shule ya sekondari Enyoito.

Wameweka wazi kuwa, wazazi wengi wamewekeza muda mwingi kwenye harakati za kutafuta kipato na kushindwa kutenga muda wa kuwafuatilia watoto wao, jambo linalowasababisha wasichana wengi kushindwa kujisimamia na kujikuta wakiingia kwenye vitendo vya ngono kwa kukosa mwongozo sahihi wa wazazi.

"Unakuta mzazi anaondoka nyumbani asubuhi, mapema kwenda kwenye shughuli zake anarudi usiku, pengine watoto wamelala, hana muda wa kuzungumza na watoto, anachojali ameacha chakula na matumizi mengine ya muhimu ya watoto, watoto wanajikuta wanajilea wenyewe ama na msichana wa kazi, jambo hili linawaangiza wasicha kwenyw ngono na kupata mimba zisizotarajiwa"wamethibitisha wasichana hao

 Waliongeza kuwa, umasikini nao unasababisha wasichana kuingia kwenye vishawishi vya zawadi na pesa kutoka kwa vijana na kujikuta wakiingia kwenye vitendo vya ngono, ili kujipatia mahitaji muhimu.

 Msichana anakuja shuleni, anatembea umbali mrefu, huku mzazi wake hajampa nauli, wala hajamlipia pesa ya chakula shuleni, kutokana na hali hiyo, wengi wanashindwa kuvumilia na kuingia kwenye mitego na vishawishi vya wanaume, na kujikuta wamebeba ujauzito na kukatisha masomo na kukatiza ndoto zao.

 Hata hivyo mtalamu wa Saikolojia na Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zena Daudi,  aliwasihi wasichana licha changamoto zinazowakabili, ikiwemo hali duni za maisha ya wazazi wao, wanatakiwa kujiamini, kujithamini na kuwa na malengo pamoja  na kujikubali na hali zao, jambo ambalo litawawezesha kuepuka vishawishi na kufikia ndoto zao, changamoto za dunia hii ni nyingi mnoo hivyo wana jukumu la kukabiliana nazo.

"Ukiwa na malengo na kujiamini na hali yako, huwezi kushawishika wala kujiona mnyonge na hali ya maisha ya wazazi wako, msichana hakikisha unajiamini, na kuridhika na maisha yako, usikubali umasikini wako ukushalilishe na kukatisha malengo na ndoto za maisha yako" amesisitiza Mwanasaikolojia Zena.

 Mdahalo huo uliendeshwa na watalamu wa halmashauri ya Arusha, kwa kushirikiana na shirika la Jhpeigo kupitia Mradi wa Tupange Pamoja, unaowezesha vijana kupata Huduma Rafiki kwa Vijana na elimi ya  afya ya Uzazi, kwa ufadhili wa Mfuko wa Bill&Melinda Gate la nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad