TRA YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA WILAYA YA KINONDONI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 18, 2020

TRA YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA WILAYA YA KINONDONI

 


Mfanyabiashara Daniel Lema akizungumza na wanahabari wakati wa baada ya uzinduzi wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Kinondoni yaliyofanyika leo Novemba 16,2020 jijini Dar es Salaam

 Kaimu Meneja wa Usajili na Uwasilishaji Ritani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Hamidy Athumani akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Kinondoni yaliyofanyika leo Novemba 16,2020 jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

 MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imetoa mafunzo juu ya maboresho mapya ya mfumo wa ritani ''return'' za kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa walipa kodi wa mkoa wa Kinondoni ili kuwawezesha kupata kuelewa  wa mfumo huo kabla ya kuanza kulipa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua mafunzo hayo Kaimu Meneja Usajili na Uwasilishaji Ritani wa (TRA) Hamidu Athumani amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu ambapo kwa sasa wameanza na wafanyabishara 500 katika wilaya kinondoni.

Amesema wanatoa mafunzo hayo kwa walipa kodi kwa kuwa, Ritani ya VAT imefanyiwa maboresho mbalimbali ikiwemo eneo la ujazaji na viambatanisho vyake hivyo ni vema wakatoa mafunzo hayo kwa wafanyabishara waliosajiliwa na VAT ili wajue namna ya ujazaji wa marekebesho katika Ritani kabla ha mfumo wenyewe kuanza kufanya kazi.

Ameongeza kuwa, kwa kupitia mfumo huo mfanyabiashara ataweza kufanya marekebisho mwenyewe ya Ritani za VAT bila ya kuandika barua kama awali ambapo huku pia maboresho makubwa yakiwa yamefanywa katika eneo la kuweka risiti za kietroniki ambazo zinakuwa hazijajazwa .

"Zamani mtu alikuwa anaweza kujaza Ritani na kuweka risiti hata kama ameiokota lakini baada ya Maboresho haya mtu hataweza kujaza Ritani katika risiti isiyokuwa ya Kwake"amesema.

Aidha Hamidu amesema, mafunzi hayo ni endelevu na wamejipanga kuwafikia Wafanyabiashara nchi nzima ambapo kwa kuanzia wameanza na Mkoa wa Kinondoni Na baadae wataenda Kariakao, Ilala na Temeke hivyo wanatarajia ushirikiano mkubwa na wafanyabiashara ili waweze kulipa kinachostahili na serikali iweze kukusanya kinachostahili.

Kwa upande wake Mfanyabiashara Daniel Lema , amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuondokana na usumbufu wa kwenda kwa Meneja mara kwa mara kujua thamani ya kodi inayodaiwa na badala yake utawarahisishia kufanya biashara zao na kulipa malipo kwa wakati na pia yatawasaidia kutambua wajibu wao na kufahamu kile wanachotakiwa kulipa.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad