MICHUANO YA CRDB TAIFA CUP YAANZA JIJINI, TIMU 36 KUCHUANA VIKALI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 12, 2020

MICHUANO YA CRDB TAIFA CUP YAANZA JIJINI, TIMU 36 KUCHUANA VIKALI

MICHUANO ya mpira wa kikapu ya "CRDB Bank Taifa Cup" imeanza rasmi katika  viwanja vya Chinangali jijini Dodoma leo Novemba 12, 2020 ambapo timu 36 za mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume na wanawake zinachuana. Pichani ni moja ya wachezaji wa Timu za Pemba (wanawake) na CRDB Youth wakichuana katika mchezo wa Utangulizi uliopigwa mchana wa leo. Picha zote na Othman Michuzi, Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB ambao ndio wadhamini wakuu wa Michuzo ya "CRDB Taifa Cup 2020", Tully Ester Mwambapa (kulia) akiwa kwenye mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV, Michael Maluwe walipokuwa wakizungumzia michezo inayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma leo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini, Phares Magesa (mwenye suti) akiwa na ugeni wake kutoka nchini Marekani uliofika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, kuangalia vipaji. 
 
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad