DKT. MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MUHULA WA PILI KATIKA AWAMU YA TANO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 5, 2020

DKT. MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MUHULA WA PILI KATIKA AWAMU YA TANO

 

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya kuapa kuwa Rais kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Tano, leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. 
Dkt. John Pombe Magufuli akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 05 Novemba 2020 katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.PICHA NA IKULU.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa Wimbo wa Taifa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu ya tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenda kukagua Gwaride mara baada ya Wimbo wa Taifa leo tarehe 05 Novemba 2020 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.


Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya Tano Muhula wa pili katika sherehe zilizofanyika leo tarehe 05 Novemba 2020 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Kikosi cha Askari wa Komando wakipita kwa ukakamavu mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Uapisho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi pamoja na Wageni Mbalimbali mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Muhula wa Pili katika Awamu ya tano leo tarehe 05 Novemba 2020 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad