Meneja wa Programu za Vijana Shirika la Childbirth Survival International(CSI) CSI, Ester Mpanda akizungumza kuhusu CSI Tanzania inavyoshirikiana na Doris Mollel Foundation wakati wa maadhimisho
Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17
ya kila mwaka yaliyofanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es
Salaam
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKA
la Childbirth Survival International(CSI) lenye makao makuu yake nchini
Marekani limeendelea kuwasisitiza Watanzania na wadau wengine nchini
kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel
Foundation katika kusaidia watoto njiti kwani malezi yao yamekuwa na changamoto nyingi.
Aidha
limesema linashukuru kwa taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation
kukubali kufanya kazi na wao kwa kuleta watu pamoja kuhusu masuala
yanayohusu afya ya mama na mtoto na kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti
Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Novemba 17 ya kila mwaka.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mbele ya viongozi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
madaktari, wauguzi na wadau wengine, Meneja wa Programu za Vijana kutoka
CSI Ester Mpanda amesema kuwa karibu na Doris kumewasaidia kujua
watoto njiti wanavyopitia changamoto nyingi katika masuala ya afya
kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati na kwamba vifo vingi vya watoto
chini ya miaka mitano ni vifo vya watoto njiti.
Katika
kuadhimisha siku hiyo ya Mtoto Njiti Duniani ,Taasisi ya Doris Mollel
Foundation iliamua kuandaa sherehe maalum iliyoambana na kuwasha taa za
zambarau katika wodi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati iliyopo
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo CSI ni miongoni mwa wadau
muhimu waliohuduria tukio hilo.
Wakati
wa sherehe hizo ,pia viongozi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Katibu wa Itikadi wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), madaktari, wauguzi na wadau wengine mbalimbali
wameungana na Doris Mollel Foundation kuadhimisha siku hiyo.
"Shirika
letu la CSI ambalo makao makuu yake yapo nchini Marekani tumejikita
zaidi katika kuangalia afya ya mama na mtoto wakati akiwa amebeba mimba
na kujifungua ,tuna programu ambazo zinawasidia wamama kujua viashiria
hatarishi.
"Pia
tumekuwa tukitoa elimu inayozungumzia mambo muhimu wanayopaswa
kuzingatiwa kwa mama aliyebeba mimba ili kubaki salama yeye na watoto
watakawaozaa, tumekuwa tukisaidia vifaa kwa kujifungulia.CSI tunazo
programu ya wasichana ambayo inayompa elimu ya kujitambua, kujielewa na
hasa masuala ya kujihusisha na ngono kabla ya umri rasmi , yote hiyo ni
kumfanya awe makini na kuanza kutambua mapema viashiria hatarishi
kuhusu masuala ya uzazi,"amesema Mpanda.
"CSI
tunawashukuru wote ambao wameungana na Doris kwa ajili ya kumsapoti,
tunaamini kumsapoti Doris ndio ni kutusapoti na sisi, huu ni mwaka
watatu tunafanya kazi na Doris ambaye amekuwa na moyo wa upendo dhidi ya
watoto njiti.
"Hivyo shirika letu ambalo limejikita katika kuhakikisha tunapunguza vifo vya
mama na mtoto, tunatoa rai kwa jamii yote kuendelea kumsaidia Doris
kwani amebeba mzigo mkubwa sana na anataka watu wote wajue umuhimu wa
siku ya leo inayotoa nafasi ya kutambua jinsi mtoto njiti anavyopata
tabu,"amesema Mpanda.
Ametumia
nafasi hiyo kwa niaba ya CSI kuwashukuru na kutambua kazi kubwa na
nzuri ambayo inafanywa na madaktari na wauguzi kote nchini ambao
wamekuwa wakitumia muda mwingi kuangalia maisha ya mama na mtoto na hasa
kuona wanabaki salama.
Amekumbusha
CSI ni shirika ambalo linajihusisha na afya ya mama na mtoto hasa
katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi kwa mama na mtoto wakati wa
kujifungua."Tuko tena hapa jioni ya leo kwasababu ya kuthibitisha kwa
vitendo jinsi CSI tunavyomuunga mkono Doris na tutaendelea."
No comments:
Post a Comment