AIRLINK YAZINDUA SAFARI MPYA DAR- JOHANNESBURG - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 30, 2020

AIRLINK YAZINDUA SAFARI MPYA DAR- JOHANNESBURG

 Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya ndege ya Airlink imezindua safari mpya za ndege kutoka Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini Desemba mosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Rodger Foster alisema wameanzisha huduma mpya kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini ili kukuza fursa za kiuchumi. 

"Airlink ina furaha kuanzisha huduma za moja kwa moja za ndege zetu ili kukuza biashara na utalii kwa kuwa sehemu hizi mbili zinafanana kwa namna moja ama nyingine katika mambo hayo," alisema.

Mbali na majiji hayo, pia abiria watapata muda wa kuunganika na miji ya Cape Town, Durban, Port Elizabert, East London, Bloemfontein na mengine ambayo ni miji maarufu kwa biashara. 

 "Katika kuhakikisha tunaonekana tofauti abiria wawapo ndani ya ndege zetu watapata huduma kama kuingia na mizigo wa kilo 20 mpaka 30 bure, chakula na kutazama madhari nzuri dirishani kwa kuwa ndege zetu hazina viti vya katikati," alisema Rodger. 

 Pia katika kuhakikisha tunakabiliana na ugonjwa wa Covid 19 kutakuwa na huduma ya vifaa vya kuchuja hewa ambavyo haviruhusu virusi kupenya na kusafisha hewa kila baada ya dakika tatu.
Airlink ikiwa imepaki uwanja wa ndege wa O.R Thambo Afrika Kusini.
Muonekano wa ndani wa ndege ya Airlink.
Huduma ya chakula.
Huduma ya vinywaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad