HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 6, 2020

TCRA yaadhimisha wiki ya Huduma Kwa Wateja

Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa wazazi kuwapeleka  watoto kutembelea  makumbusho  ya mawasiliano  yanayoelezea maendeleo na ukuaji wa teknolojia  za mawasiliano duniani na hakuna gharama ya kuingia katika Makumbusho hayo ni bure.

TCRA  inaadhimisha wiki ya huduma kwa  wateja  kwa kutoa wito  kwa wazazi na shule  pamoja na wananchi kwenda katika makumbusho ya Mamlaka kujifunza vitu mbalimbali vilivyotumika katika Mawasiliano kabla ya ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano haijaanza.

Katika Maadhimisho hayo Mamlaka imejenga  dawati maalum la kuhudumia wateja kutokana na huduma wanazozitoa.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mabel Masasi amesema Maadhimisho hayo wanatarajia kupata  maoni yao katika utoaji wa huduma kwa Mamlaka na kuangalia kujipanga katika mikakati.

Amesema Maadhimisho hayo ya huduma kwa wateja hufanyika kwa mwaka mara moja hivyo ni fursa ya wadau kujitokeza  na kutoa maoni

"Tunaendelea kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja tukilenga kupata maoni yao na kutembelea katika dawati maalum lililoanzishwa kwa ajili hiyo"amesema Mabel.

Hata hivyo katika kuadhimisha Maadhimisho hayo kuna mikakati mbalimbali imewekwa kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora za Mawasiliano.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akimpa mwanachi kitabu cha muongozo cha huduma kwa wateja  aliyetembelea Wiki ya Huduma kwa Wateja Makao Makuu ya Mamlaka hiyo  Barabara ya Samnujoma jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata maelezo katika Makumbusho ya TCRA walipotembelea mamlaka hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dorice Mhimbila akimhudumia mwananchi wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka hiyo katika wiki huduma kwa wateja Duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad