Tanzania Kutumia Maonesho Makubwa ya Qatar Kutangaza Utalii - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 14, 2020

Tanzania Kutumia Maonesho Makubwa ya Qatar Kutangaza Utalii

 

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab alikutana na Shirika la Qatar Travel Mart (QTM) linalojishughulisha kutangaza utalii wa ndani na nje ya Qatar pamoja na kuandaa Maonesho ya Utalii. Shirika hilo linajiandaa kufanya Maonesho Makubwa ya Utalii yatakayofanyika tarehe 17-19 November 2021. Mataifa mengi ya kigeni ya Asia, Ulaya na Marekani yanatarajiwa kushiriki Maonesho hayo pamoja na ofisi za Kibalozi ziliopo Qatar.

Maonesho hayo yatatoa fursa kwa nchi kutangaza Biashara, uwekezaji na Sanaa. Mhe. Balozi amewaahidi kuwa Tanzania itashiriki kikamilifu kwenye Maonesho hayo. Aidha kabla ya Maonesho hayo Ubalozi utaandaa Mkutano wa Mtandao Webinar Conference mwezi Desemba 2020 baina ya Shirika hilo la QTM na TTB na ZTC ili kuelezea vivutio vya Utalii vya Tanzania na kukaribisha watalii kutoka Qatar
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad