HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 20, 2020

SIKU YA MUONGOZAJI NDEGE DUNIANI; TANZANIA YAADHIMISHA KWA KUTEMBELEA GEREZA LA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Vallery Chamulungu akizungumza na wanahabari pamoja na waongoza ndege katika maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam.

Katika Maadhimisho hayo Chama cha Waongoza ndege Tanzania (TATCA) kimefanya mafunzo mafupi ya kuwajengea uwezo wanahabari ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa vyereheni 4 pamoja na mashine ya kufuma katika Gereza Kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam. Siku ya muongozaji ndege duniani huadhimishwa oktoba 20 kila mwaka. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Usafiri wa Anga TCAA Redemptus Bugomola  akizungumza katika maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Kuongoza ndege (TCAA) Justin Ncheye akizungumza katika maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam.
Waongozaji wa ndege wakifuatilia maadhimisho ya siku ya muongozaji ndege duniani iliyofanyika makao makuu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) Shukuru Nziku (kulia) akitoa msaada kwa Mkuu wa Gereza Kuu la Ukonga Salumu Manjawa (Kushoto) vyereheni 4 pamoja na mashine ya kufuma ili viweze kuwasaidia wafungwa kushona nguo zao. Wengine ni maaskari wa magereza na waongoza ndege.
Waongoza ndege na Askari wa Magereza wakiwa katika picha ya pamoja. 
Waongoza ndege wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad