CCM MKOA WA SINGIDA KUANZISHA MAKTABA YA VITABU VYA NYERERE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 15, 2020

CCM MKOA WA SINGIDA KUANZISHA MAKTABA YA VITABU VYA NYERERE

 CCM MKOA WA SINGIDA KUANZISHA MAKTABA YA VITABU VYA NYERERE

Na Ismail Luhamba, Singida.

KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida,  Ahmed Kaburu amesema Chama hicho kinampango wa kuanzisha maktaba ya vitabu vya Mwalimu.Nyerere ili kuwawezesha vijana kuzijua fikra za kizalendo alizokuwa nazo kupitia vitabu hivyo.

Kaburu aliyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya siku ya kumbukizi ya Miaka 21 ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo alimwelezea kwa namna alivyokuwa na uzalendo na Taifa lake.

"Mwalimu Nyerere alifanya mambo makubwa,alituunganisha sisi watanzania kwa kuondoa ukabila,udini na kufanya sisi sote tuzungumze lugha moja haya yote ni kutokana na uzalendo wake,na sisi hapa Singida tunamkumbuka kwani hata jengo letu la CCM Mkoa yeye ndio aliweka jiwe la msingi,hivyo vijana wanapaswa kuiga uzalendo huo." alisema Kaburu.

Alisema lengo la maktaba hiyo ni kuwawezesha Vijana wote ambao hawakubahatika kumfahamu Baba wa Taifa na vizazi vijavyo kumfahamu kupitia vitabu mbalimbali vinavyomwelezea na kumzungumzia Mwalimu,na maktaba hiyo sio kwa wanaCCM tu bali ni kwa Vijana wote.

Aliwataka Vijana kuzingatia suala la maadili katika jamii inayowazunguka ili kuendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere kwani alikuwa ni mtu anayejali maadili,hakutaka kabisa maadili kuporomoka.

Aidha aliwaomba wananchi wa mkoa huo kutorubuniwa na baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa wanaobeza mafanikio yaliyofanywa na Serikali badala yake wayapime wao wenyewe kwa kuyatazama yaliofanyika.

"Kuna baadhi ya wagombea wanabeza mafanikio yaliyofanywa na Magufuli kwa kudai hajafanya chochote, nawaomba wananchi pimeni nyie wenyewe sio kwa kurubuniwa." alisema Kaburu.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad