Benki ya NMB Kutoa Mikopo Nafuu kwa Wakulima na Wafanyabishara - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 15, 2020

Benki ya NMB Kutoa Mikopo Nafuu kwa Wakulima na Wafanyabishara

 

Benki ya NMB imesema kuwa imejipanga kuhakikisha inawasaidia wakulima na wafanyabiashara wadogo na wakubwa, katika kukuza shughuli zao za kiuchumi wanazozifanya kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili waweze kunufaika na shughuli wanazozifanya.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB – Alex Mgeni katika kongamano la wafanyabiashara NMB Business Club lililowakutanisha wadau mbalimbali zaidi ya 900 wakiwemo wajasilimali, wakulima na wafanyabiashara kutoka mikoa mitatu ya Njombe, Iringa na Mbeya katika ukumbi wa Green City mjini Makambako.

Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB - Alex Mgeni akielezea namna Benki hiyo imejipanga kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara ili kupata mikopo nafuu.

Akifafanua zaidi kuhusu mikopo ambayo inatolewa na Benki hiyo kwenye sekta ya kilimo kwa ajili ya Kilimo biashara, Meneja Mwandamizi Idara ya Kilimo,Wogofya Mfalamagoha alisema, Benki ya NMB inatoa mikopo ya vifaa kwaajili ya shughuli za kilimo ikiwemo trekta na mashine za kuchakatia mbao kwa masharti nafuu na inalipwa kwa miaka mitatu na kila mwaka mkulima analipa mara moja baada ya mavuno.


Meneja mwandamizi Idara ya kilimo- Wogofya Mfalamagoa akitoa elimu ya mikopo inayo tolewa na Benki ya NMB kwenye sekta ya kilimo.

Aidha, Meneja huyo alifafanua kuwa katika kuhakikisha mkulima ananufaika na shughuli ya uzalishaji wa mazao, Benki hiyo inatoa mkopo kwa mkulima ili aweze kujegha ghala la kuhifadhia mazao yake wakati anasubiri kuuza kwa bei zenye tija. Pia wakulima wadogo wadogo waliopo kwenye vikundi wanawezeshwa kwa kupatiwa mikopo na elimu ya shughuli wanayoifanya.

Naye meneja wa mikopo Benki ya NMB tawi la Makambako - Kenneth Hankungwe alisema kuwa Benki hiyo kwa sasa inatoa huduma za mikopo ya nyumba, ambayo inamuwezesha mwananchi kununua nyumba ya makazi, kujenga nyumba na inatoa mkopo wa fedha kwa mfanyabiashara ambaye biashara yake imeyumba kutokana na kutimia fedha hizo kwenye ujenzi, huku akieleza kuwa mikopo ya nyumba inatolewa kuanzia milioni 10 hadi milionI 700 inayolipwa katika kipindi cha miaka 15.
Mwenyekiti wa NMB Business Club Mafinga - David Mdeka akiishukuru NMB kwa huduma bora wanazo zitoa.

Hata hivyo baadhi ya wanachama wa NMB Business Club – Kanda ya Nyanda za juu wameishukuru Benki hiyo kwa kuwajali, kuwapa elimu kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zikiwemo; NMB mkononi na Bima(Bancassurance) itakayopelekea shughuli zao kukua.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad