HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 9, 2020

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUZINDUA MPANGO MKAKATI WA KIDIGITALI WA AFYA

 

 Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma akitoa tarifa kuhusu uzinduzi wa mpango mkakati wa Kidigitali wa Afya unaotarajiwa kuzinduliwa Septemba 10 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Mafunzo wa Wizara ya Afya Mwinyi Msellem akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Mpango Mkakati wa wa Kijitali wa afya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.


Na Ramadhani Ali – Maelezo 08,09,2020
WIZARA ya Afya itazindua Mpango Mkakati wa Kidigitali wa Sekta ya Afya utakaoweka mifumo bora ya uimarisha wa huduma za Afya kwa wananchi wa Zanzibar kuanzia mwaka huu.

Mpango huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Afya Hamad Rashid Muhamed tarehe 10 mwezi huu katika Hoteli ya Verde iliyopo Mtoni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi wa Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma amesema Mpango huo wa miaka mitano utapunguza gharama kwa Serikali na wagonjwa. 

Ameweka wazi kuwa Mpango huo utaimarisha upatikanaji wa huduma na utarahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za wagonjwa ambazo zitasaidia uongozi wa Wizara kutoa maamuzi yaliyo sahihi ya afya katika wakati muafaka.

Aidha amesema Mpango huo wa Kidigitali utaweka kumbukumbu zote muhimu za wagonjwa watakaofika hospitali kupata huduma kwa njia ya kijitali kutoka hospitali na vituo vyote vya afya.

Amewahakikisha wananchi kuwa Serikali imejipanga kikamilifu na wanauhakika kuwa mpango huo utaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya afya.

Mkurugenzi wa Mafunzo wa Wizara ya Afya Mwinyi Msellem alieleza kuwa Mpango Mkakati wa huduma za afya Zanzibar utasaidia kulinda maadili na utaongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wagonjwa.

Alisema baada ya kumalizika kipindi cha miaka mitano Mpango huo utafanyiwa mapitio ili ikionekana kulikuwa na mapungufu katika utekelezaji yaweze kufanyiwa kazi.

Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa Wizara ya Afya Mohamed Habib amesema Mpango huo pia utasaidia sekta nyengine nyengine muhimu za Serikali ikiwemo sekta ya elimu.

Aidha alisema katika kuhakikisha Mpango huo unakuwa wa mafanikio, wameandaa mifumo mbadala ya upatikanaji wa miundombinu ya dharura ikiwemo huduma ya umeme na mitandao ya simu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad