HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 4, 2020

RAIS MAGUFULI ATAJA SABABU YA KUANZA NA VITU VINAVYOCHOCHEA UCHUMI WA NCHI

 


Na Said Mwishehe, Michuzi TV –Simiyu

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dk.John Magufuli amesema ili kuwa na uchumi imara katika nchi lazima uanze na vitu vinavyochochea uchumi.

Dk.Magufuli amesema hayo leo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu unaotatarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema katika nchi yoyote ukitaka kujenga uchumi ni lazima uanze na vitu vinavyochochea uchumi, huwezi kutaka kujenga uchumi wakati vitu vinavyochochea uchumi havijaendelezwa,

“Hata Mungu mwenye alipotaka kuiumba Dunia hakuanza  na watu, alianza na ardh ili watu waje waitumie kulima,akaleta jua ,a akaleta dunia baadae akaleta wanyama na ndege ili  binadamu watakapokwenda katika ardhi ile wakaiwatawale na alitumia siku sita na ya  saba akampumzika,”amesema Dk.Magufuli

Hata hivyo amefafanua mbele ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwamba alipoingia madarakani aliona atumie mbinu ya kujenga uchumi wa kisasa katika nchi hii na ndio maana walianza na miundombinu na anakumbuka hata Bariadi watu walikuwa wanakufa bila kutibiwa hospitali na walikuwa wanabebwa kwenye tela za ng’ombe.

“Mmesahau, tukasema lazima tujenge hospitali kubwa ya Rufaa itakayofanya upasuaji wa aina zote, wakati nakwenda kuweka jiwe la msingi watu hawakuwamini kama kutakuwa na hospitali ya rufaa , leo pale Itilima, leo haa Bariadi hospitali ipo,

Wakati anaingia madarakani hii barabara haikuwepo na anakumbuka wakati anabomoa nyumba zilizokuwepo kwenye hifadhi ya barabara alisema ipo siku moja watu wa Simiyu watafurahi.”Tumejenga miundombinu ya barabara ili kutengeneza uchumi wa kisasa”.

Akizungumza zaidi na wananchi wa Simiyu  amewaahidi kwamba wakimchagua tena miaka mitano mingine atahakikisha ndani ya miaka mitatu vijiji vyote kijiji kitakuwa na umeme kwani tayari vijiji zaidi ya 10,000 tayari vina umeme na vibaki vijiji 2600.

“Nataka kusema hili Simiyu, sitaki kusema mbele ya Mungu, mkitupa miaka mingine mitano nina uhakika kama mitatu vijiji vyote vitakuwa na pa umeme, ndio maana nakuja kuwaomba kwanini watu wafanye majaribio hatawatufikisha mahali.

“Tumehangaika wote, tumebana mafisadi wote, tumeanza viruzi, ndio maana nafikiri watu wa Bariadi na Simiyu mnipe kura ili tuendelee,”amesema Dk.Magufuli wakati anazungumza na wananchi hao.
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dk.John Magufuli

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad