HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 28, 2020

PROFESA MANYA ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

 

 

Tarehe 27 Septemba, 2020 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya ametembelea mabanda ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji Bombambili Geita Majini .
Mara baada ya kutembelea Banda la Tume ya Madini kwenye maonesho hayo amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wataalam wa Tume na kuwataka kuendelea kuelimisha umma  hasa wachimbaji wadogo kuhusu Sheria ya Madini na kanuni zake, usalama wa afya na mazingira wanapoendesha shughuli za uchimbaji wa madini na biashara ya madini.

Aidha ameelekeza elimu kuhusu ushirikishwaji wa watanzania kwenye Sekta ya Madini kuendelea kutolewa ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki kwenye sekta ya Madini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad