HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 29, 2020

NEC YAVITAKA VYAMA VYA SIASA KUZINGATIA MAADILI NA KUEPUKA UCHOCHEZI


 


TUME ya Taifa ya Uchaguzi NEC imevitaka Vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Urais,Wabunge na Madiwani kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kipindi cha kampeni zao ikiwemo kuepuka lugha za kashfa ,maneno ya uchochezi ambayo yanayotishia Amani ya nchi.

Wito huo umetolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mh Jaji Mstaafu Mbarouk S.Mbarouk wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa uchaguzi Mkoa wa Dodoma.

"Aidha kunapokuwa na malalamiko yoyote ya kimaadili basi hatua stahiki zichukuliwe ikwemo kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliowekwa’’ Amesema.

Aidha amesema Tume inaendelea kusimamia na kuendesha uchaguzi kwa kutumia sheria za uchaguzi hivyo vyama vya siasa,wagombe na wananchi wanakumbushwa kuwa  katika kipindi hiki sheria nyingine za nchi hazijasimama  hivyo wanapaswa kujihadhari na vitendo ama matamshi ambayo kusababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.

"Tume inawahakikishia wananchi kuwa imejipanga katika kusimamia uchaguzi wa mwaka huu kwa kufuata katiba sheria,kanuni na miongozo mbalimbali na inaimani kuwa kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kufuata taratibu watanzania wataweza kupiga kura kwa amani siku ya uchaguzi’’Amesema

Katika hatua nyingine tume imewatoa hofu wapiga kura  wenye mahitaji maalumu kuwa maelekezo yametolewa kwa watendaji wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu,wajawazito,akina mama wanaonyonyesha waliokwenda na watoto vituoni,wazee na wagonjwa.

"Kwa wasio jua kusoma na kuandika wanaruhusiwa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura ,aidha kwa watu wenye ulemavu wa kuona kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na kifaa cha maandishi ya nukta nundu  Tictile ‘’Ballot Folder’’ hiyo ni kwa wale wanafahamu kutumia maandishi hayo na kwa wasioweza wataruhusiwa kwenda kituoni na mtu anayemwamini wakuweza kumsaidia" Amesema

Hata hivyo, Jaji Mbarouk amesema kwa wenye ulemavu wa viungo vituturi vitakavyotumika kupigia vinaruhusu kuwahudumia kwani kuna pande mbili tofauti ambapo upande mmoja kuna urefu wa kutosha na kikigeuzwa kinakuwa kifupi kumuwezesha mwenye ulemavu wa viungo kupiga kura.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad