HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 September 2020

MJENGONI CLASSIC BAND KUSIMAMISHA MJI WA TABORA

 Na Woinde Shizza, michuzi TvArusha

BENDI maarufu hapa nchini inayojulikana kwa jina la mjengoni Classic band yenye makazi yake mkoani Arusha inatarajia kutua mkoani Tabora kutoa burudani katika ukumbi wa Club Inferno mapema September 25 na 26 mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdeme alisema kuwa bendi hiyo inatarajia kusimamisha mji huo na wapenzi wao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo.

Alisema kuwa wamejipanga vyema kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa mkoa huo mzima pamoja na mikoa jirani na kwa upendeleo watawatambulisha nyimbo zao mbalimbali ambazo wameziandaa na zinazotamba kwa sasa.

Alisema kuwa timu yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi itakayo wafurahisha wakazi wa mkoa mzima kwani hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii ya mjengoni kutoa burudani mkoani hapo.

Kwa upande wake Rais wa bendi hiyo Digital Mukongya (TIGER) alisema kuwa atawapa staili zote za bendi hiyo ikiwemo ile ya bichwa kubwa ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha zaidi na ina vinjonjo vingi zaidi, staili tamu pamoja na maneno matamu.

“Tunatarajia kufanya show ya kihistoria ambayo aijawai kufanyika au kufanywa na bendi yeyote ile mkoani Tabora yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha wapenzi wetu wa mziki wa dance wapenzi wetu wa bendi yetu ya mjengoni classic bandi”alisema Digital

Aidha alisema kuwa amewaandalia zawadi kubwa wapenzi wake wa mkoa wa huo pamoja na mikoa jirani kwani watamuoana namna nyimbo zao zinavyochezwa ikiwemo kuwaona wanenguaji wao namna wanavyojua kulicheza sebene pamoja na kushuhudia namna nyimbo zao zinavyochezwa

“Niwaambie tu wakazi wa mkoa wa Tabora kuwa kikosi kizima cha bendi ya mjengoni kitakuwepo na tutatoa buradani ya kufa mtu ,yaani tutatoa burudani zaidi ya tulivyotoa katika mikoa mingine tulioenda kama dar es salaam,Dododa,Mwanza na penginepo nachotaka niwasisitize tu wasiache kuja katika siku hiyo ya shoo waje wajionee burudani ya nguvu”alibainisha Digital."


Wanamziki bendi ya mjengoni classic band wakiongozwa na Rais wao Digital Mukongya (TIGER) wakiwasha Moto katika ukumbi wa Hugo's mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki hii.
Picha na Woinde Shizza

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad