HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 12, 2020

MGOMBEA UDIWANI NEGRO SANGA KATA YA IKONGOSI ITAKUWA NA MAENDELEO MAKUBWA MIKA MITANO IJAYO

Mgombea udiwani wa kata ya Ikongosi Negro Sanga akiomba kura kwa wananchi wa kijiji cha Mtili kwa ajili ya mbunge na Rais kwa kuwa yeye kama mgombea udiwani wa kata hiyo amepita bila kupingwa.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo wa kampeni za chama cha mapinduzi za kuomb kura za mbunge na Rais kwenye kata ya Ikongosi kijiji cha Mtili

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa kata ya Ikongosi wanategea kupata maendeleo makubwa kwa miaka mitano ijayo kutokana na mikakati aliyokuwanayo mgombea udiwani wa kata ya Ikongosi Negro Sanga wakati akiomba kura za Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuwa yeye ameshapita bila kupigwa.

Hayo yalisemwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mtili kilichopo kata ya Ikongosi kwa kutoa ahadi ya kukamilish ujenzi wa ofisi ya kata kwa kuwa kila kitu kipo kwenye mipango dhabiti kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.

Sanga alisema kuwa wanatarajia kuwa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi itajengwa katika kata ya Ikongosi kwa kuwa mchakato wote ulishafanyika kwenye baraza la madiwani lilolopita hivyo wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa zitakazo jitokeza hapo baadae.

Alisema kwa miaka mitano iliyopita maendeleo mengi na makubwa yamefanyika katika kata hiyo kwenye sekta ya afya,miundombinu kama barabara,majengo,sekta ya michezo,elimu,kilimo na biashara hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi kwa utekeleza wa Ilani yake.

“Miaka mitano mliyonipa ridhaa ya kuwa diwani wenu kwa ushirikiano mkubwa tumefanya kazi kubwa ya kujenga Ofisi za vijiji kwenye vijiji vyote vitano tena kwa ubora mkubwa na sasa kwa pamoja tunatekeleza ujenzi wa ofisi ya kata” alisema Sanga

Aidha Sanga alimuomba mgombea ubunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe kutengeneza ushirikiano ulitukuka kwa wabunge zenzake wa wilaya ya Mufindi kwa lengo la kusaidiana kuleta maendeleo kwenye wilaya ya Mufindi ambavyo inautajili mkubwa.

Mgombea udiwani huyo alimalizia kwa kumshukuru mbunge aliyemaliza muda wake Mahmoud Mgimwa kwa ushirikiano wa kimaendeleo alioutoa kwenye kata hiyo kwa kipindi chote alichokuwa madarakani kwenye jimbo la Mufindi Kaskazini.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazinikupitia Chama cha Mapinduzi (CCM),Exaud Kigahe alisema kuwa jimbo laMufindi Kaskazini linakabiriwa na changamoto ya miundombinu ya Barabara ambazozimekuwa hazipitiki kwa msimu mzima hivyo akipewa ridhaa ya kuwa mbungeatahakikisha anatatua kero hiyo.

Alisema kuwa atahakikisha anaboresha sekta ya Elimu kwa kujenga na kukarabati majengo ya shule,kuanzisha mashindano ya kumpata mwananfunzi bora namwalimu bora kwa atakayefanya kazi nzuri ya kuwasaidia wanafunzi kufaulu kwawastani mzuri.

“Wananchi wa jimbo la Mufindi wengi niwakulima hivyo siwezi kuisahau sekta ya kilimo kwa kuwa hata mimi nimekuliakwenye family ya wakulima hivyo nitahakikisha kuwa tunaboresha masoko ya wakuliwa ili waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri” alisema Kigahe

Aidha Kigahe alisema kuwa ahadi nyingine ni pamoja na viwanda,afya,biashara,umeme na michezo ambazo atazifanyia kazi kama akiwambunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Kazi kubwa mliyonipa nitaifanya kwa nguvu naniwahakikishie sisi wabunge watatu wa Wilaya ya Mufindi (Kihenzile na Chumi) tutafanya kazi kwa pamoja kwa kuwa lengokubwa ni kuleta maendeleo”alisema Kigahe


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad