HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 21, 2020

MERIDIAN BET, LIONS CLUB WAWAPIGA TAFU WAZEE KINYEREZI

 KAMPUNI ya Mchezo wa Kubahatisha ya Meridian Bet, Lions Club na Kituo cha Jamii cha Tiba ‘CCP Medicine’, wameandaa mradi wa kusaidia wazee hapa nchini utakaotekelezwa kwa miaka mitano kuanzia sasa.

Jumapili ya Septemba 20, 2020, Meridian Bet na Lions Club, ilitoa misaada ya vyakula kwa wazee wanaoishi Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Miongoni mwa misadaa hiyo ni unga, mchele, chumvi na mito.

Msaada huo ni katika kuunga mkono juhudi za kuwasaidia wazee kuelekea Siku ya Wazee Duniani ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi ya kila mwaka.

Amani Siaforo Maeda kutoka Meridian Bet, alisema: “Tumeanza kwa kutoa hivi leo, itakuwa mwendelezo na tutakuwa tukitoa kwa wazee mbalimbali.”

Naye Mratibu wa Lions Club, Rizwan Kadri, alisema kwa kushirikiana na Meridian Bet, wameamua kuwashika mkono wazee na kuwatia faraja kupitia misaada hiyo.

Dokta Manase kutoka CCP Medicine, aliwashukuru Meridian Bet na Lions Club kwa kusema: “Tunawashukuru Meridian Bet na Lions Club kwa kutoa muda wao ili kushiriki katika kuwafariji wazee wetu kwa kuwapatia mahitaji muhimu ambayo yataweza kufariji katika maisha yao.

“Kutokana na utafiti tulioufanya, tumekusudia kutokomeza matatizo ya kiafya yawapatayo wazee kiafya, kisaikolojia, kihisia na kiroho ili kuwaboreshea maisha yao.

“Wazee wanahitaji malezi, makazi bora, afya bora na mawasiliano mazuri. Tunatoa tiba za aina mbalimbali kama vile tiba ya kisaikolojia, kisanaa, kimuziki na tiba ya lishe itakanayo na wanyama na mimea ambayo imeonesha matokeo chanya ya kuponesha ukilinganisha na dawa.


Picha ya Pamoja.

14 comments:

  1. Ni jambo la kher pia kwa kurudisha fadhila kwa jamii

    ReplyDelete
  2. Jambo zuri sana kutoa msaada kwa wenye uhitaji

    ReplyDelete
  3. Ni Jambo zuri sana kutoa msaada kwa wenye uhitaji

    ReplyDelete
  4. Ni Jambo zuri la kuigwa sana kwa meridianbet kuona n vzur kujitoa kwa kiasi kuwasaidia wasiojiweza hongera sana 👍

    ReplyDelete
  5. Hili ni jambo la kuigwa kwa washikadau wote hapa nchini, Pongeza kwa Meridianbet na Lions Club

    ReplyDelete
  6. Safii hii nzuri sana kuwakumbuka wazee wetu ni jambo la kher

    ReplyDelete
  7. Safii sana kwa utu wenu wakujali wale wanao hitaji mahitaji kutoka kwenu

    ReplyDelete

Post Bottom Ad