
Mgombea
Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (kushoto) akizungumza
na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi wa Tarafa ya
Mkamba.(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)


Wananchi wakimsikiliza mgomea ubunge jimbo la Mkuranga.

Mwanachama mpya wakipokea Kadi za CCM
WANANCHI
wa tarafa ya Mkamba wilayani Mkuranga mkoani Mkuranga Pwani wameahidiwa
kupatiwa gari ya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya mkamba kilicho
boreshwa ikiwa ni pamoja na kujaziwa vifaa, na kuletewa daktari wa
upasuaji ili kuendelea kutoa huduma bora.
Aahadi
hiyo imetolewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri
wa Mifugo Na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya kampeni katika Kata
ya Mkamba, Pupu na Panzuo zilizopo katika tarafa ya mkamba na kusema
kituo cha afya Mkamba kilikuwa na halimbaya wakati anaingia madarakani
lakini kwa juhudi za Daktari John Pombe Magufuli Sasa kimeboreshwa.
Ulega
amesema ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kupitia ilani ya
chama cha mapinduzi ya mwaka 21/25 kila kituo cha afya nchini
kitapatiwa gari kwa ajili ya kubebea wagonjwa.
Kwa
upande mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mkuranga,Ally Msikamo aliposimama
kuwaombea kura wagombea wachama cha mapinduzi akiwemo Rais, mbunge na
diwani amesema
Hata
hivyo Ulega amesema anaenda kuinua kiwango cha elimu mkamba kwa kujenga
Shule ambapo ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni tano kwa
ajili ya ujenzi wa shule ya Nyekenge, lengo nikuhakikisha Mkamba inapata
wasomi wengi.
No comments:
Post a Comment