Tanzania
public Health Bulletin (TPHB) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wamekutana na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam na kutoa mafunzo maalumu kuhusiana na
namna bora ya kuripoti habari za afya ambapo kupitia mradi wa Takwimu na
Sera za afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, Wizara ya afya,
Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na ofisi ya mganga
mkuu wa Serikali wamerahisisha namna ya kupata taarifa muhimu za afya
kupitia jarida la Afya ya Jamii nchini, ambalo limesheheni taarifa na
matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kutoka Wizara ya Afya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara Kuu ya Afya Gerald Chami
akizungumza na wanahabari wakati wa mafunzo maalumu ya kuwajengea
wanahabari uwezo wa namna ya kuripoti habari za afya, ambapo ameeleza
kuwa Wizara hiyo imetengeneza daraja baina yao na waandishi wa habari
ili wananchi waweze kupata taarifa muhimu za afya kwa wakati, leo jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Uratibu na Ukuzaji Tafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mary Mayige akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa mafunzo ya maalumu ya kuwajengea uwezo wanahabari
katika kuripoti habari za afya, ambapo amesema kuwa Mamlaka hizo zipo
tayari wakati wowote katika kutoa taarifa na ufafanuzi, leo jijini Dar
es Salaam.
Kaimu
Mhariri mkuu wa Jarida la Afya ya jamii Tanzania (TPHB) Dkt.Julius
Massaga akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusiana na namna ya
kuripoti habari za afya na kueleza kuwa kupitia jarida hilo la Afya
wananchi, wanahabari na watunga sera watapata fursa ya kupata majibu ya
maswali yao kupitia tafiti mbalimbali zilizochapishwa katika jarida
hilo, leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi
wa habari kutoka Michuzi Blog Leandra Gabriel akipokea cheti cha
ithibati na pongezi mara baada ya kufuzu mafunzo hayo yaliyofanyika kwa
siku mbili, leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi
mbalimbali kutoka TPHB, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari
walioshiriki mafunzo hayo, leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment