WALIOSHINDWA KUZIFUATA HATI ZA ARDHI BUNDA WAMKERA NAIBU WAZIRI MABULA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 10, 2020

WALIOSHINDWA KUZIFUATA HATI ZA ARDHI BUNDA WAMKERA NAIBU WAZIRI MABULA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Ardhi mkazi wa Nyasula wilay ya Bunda mkoa wa Mara Bi. Tausi Sono wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara jana. Kulia aliyesimama ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Jerome Kiwia.


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Bunda na wananchi aliowakabidhi Hati za Ardhi wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara jana.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi wa ofisi ya ardhi mkoa na Manispaa za wilaya ya Musoma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara jana. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Mara Jerome KiwiaBaadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoa wa Mara jana.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati ya Ardhi Mwakilishi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania wilaya ya Rorya Musa Hamis wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara mwishoni mwa wiki (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

…………………………………………………………………..

Na Munir Shemweta, WANMM BUNDA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshangazwa na wananchi wa wilaya ya Bunda waliomilikishwa ardhi kushindwa kujitokeza kuchukua hati pamoja na kutangaziwa siku ya kukabidhiwa hati zao.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanzisha utaratibu kupitia ofizi zake za mikoa kuwapelekea Hati wananchi karibu na maeneo yao ili kuwapunguzia usumbufu wa kuzifuata hati kwenye ofisi za mikoa.

Awali waliomilikishwa ardhi walitakiwa kusafiri umbali mrefu kufuata hati za ardhi ofisi za ardhi za kanda zilizokuwa zikihudumia mikoa zaidi ya mitatu jambo lililowafanya wamiliki hao kutumia gharama kubwa kufuatilia hati ofisi ya kanda.

Katika kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi pamoja na kupunguza gharama kwa wananchi kuzifuata huduma hizo kwa umbali mrefu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Julai mwaka huu imezindua ofisi za ardhi za mikoa zinazotoa huduma zote zilizokuwa zikitolewa katika ofisi za kanda. Huduma hizo ni pamoja na upimaji, uthamini, usajili na utoaji hati za ardhi pamoja na shughuli za mipango miji.

Akiwa wilayani Bunda jana katika ziara yake ya kikazi kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na miradi inayoendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa, Naibu Waziri Ardhi Dkt Mabula alishangazwa na idadi ndogo ya wananchi waliomilikishwa ardhi kujitokeza kuchukua hati zao wilayani Bunda ambapo kati ya wamiliki 143 ni wamiliki sita (6) tu kati ya hao waliojitokeza kuchukua hati.

Naibu Waziri Mabula alisema, inashangaza kuona idadi ndogo ya wamiliki wa ardhi kujitokeza kuchukua hati wakati Wizara ya Ardhi imeamua kuwapelekea hati karibu na maeneo jambo linaloweza kuwasababisha kutumia gharama kuzifuata hati ofisi ya Msajili katika ofisi ya Ardhi mkoa wa Mara.

Katika ziara yake mkoani Mara Dkt Mabula alitembelea pia wilaya za Butiama, Tarime, Rorya na Musoma ambapo alizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika wilaya hizo, kuangalia ukusanyaji kodi ya ardhi sambamba na kugawa Hati za Ardhi kwa wananchi waliokamilisha taratibu za kumilikishwa ardhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad