Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano
kwa wote (UCSAF) umekutana na wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa
wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa huduma za
usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni kwa lengo
la kuwajengea uelewa watoa huduma na wadau hao kushiriki shughuli za
mfuko wa UCSAF na kutimiza wajibu wao kisheria.
Akizungumza
katika Mkutano huo leo Agosti,31 2020 uliofanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala
UCSAF, Pius Joseph alisema mkutano ulilenga kuwajengea uelewa wadau wa
mawasiliano namna mfuko wa UCSAF unavyofanya kazi na wajibu wao
kisheria.
Joseph
aliyataja miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa na mfuko wa UCSAF ni
pamoja na kufikisha huduma ya mawasiliano ya simu katika kata 631 kati
ya kata 994 zilizosainiwa mkataba,ufikishwaji wa matangazo ya runinga ya
kidigitali katika mikoa ya Katavi, Geita,Simiyu,Njombe na Songwe pamoja
na ujenzi wa vituo 10 vya TEHAMA Zanzibar na 11 Tanzania bara ambapo
kituo kimoja kimejengwa katika kila wilaya.
Hata
hivyo alisema suala la ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi unaathiri
kasi ya mfuko kufikisha mawasiliano,ukosefu wa fedha za kutosha
kufikisha mawasiliano kwa kipindi kifupi zaidi kulingana na mahitaji na
uelewa wa watoa huduma na wadau mbalimbali kushiriki shughuli za mfuko
na kutimiza wajibu wao kisheria.
Joseph
aliwashauri wamiliki wa vituo vya utangazaji kushirikiana kujenga
minara ya pamoja ili kupunguza gharama za kuendesha vituo vya matangazo
na kwamba UCSAF inachofanya ni kuwawezesha watoa huduma kwa kuwapa
ruzuku ili kujenga minara.
Kwa
upande wake, Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye
ni Mjumbe wa Bodi ya UCSAF alisema upenyo wa kuenea kwa vyombo vya
habari kanda ya Ziwa bado hauridhishi ambapo usikivu wa redio Kanda ya
Ziwa upo chini ya asilimia 50 hivyo kuwaomba Watoa huduma za mawasiliano
kuomba Ruzuku UCSAF kwa ajili ya kujenga minara ya pamoja ili walau
usikivu ufikia asilimia 60.
“Mkijenga
minara maeneo mengine,kama kuna mnara umejengwa na wadau wa sekta ya
utangazaji,gharama zitapungua. Tuache ubinafsi tutumie minara
iliyojengwa kwa ruzuku ya serikali. Lengo tunataka kuongeza usikivu wa
radio Kanda ya Ziwa”,alisema Mhandisi Mihayo.
"Kuna
watu wanawafanya nyinyi kama vitega uchumi, akili kubwa mnaelekeza
kulipia kodi ya minara ili msizimiwe matangazo,hao wanaowapangisha
silaha yao kubwa ni kuzima matangazo. Nawasihi wamiliki wa vituo vya
utangazaji kuungana.
Tumieni
nafasi hii mji – organize, leteni maombi UCSAF kujenga mnara wa pamoja
ili kupunguza gharama za uendeshaji wa vituo vyenu tuache wivu na
ubinafsi. Jengeni na kumiliki vya kwenu kupitia ruzuku ya serikali,
tunataka mjenge wote, utakachotakiwa kufanya ni utachangia umeme na
kulipa mlinzi tu”,aliongeza Mihayo.
Hata
hivyo Mjumbe wa Bodi ya UCSAF, Samweli Nyalla alisema lengo la UCSAF
kuhamasisha watoa huduma za mawasiliano kujenga minara ya pamoja ni
kutaka kupeleka matangazo sehemu ambazo hakuna mawasiliano.
"Sasa
hatuangalii pale ulipo,tunaangalia kule ambako hufiki,kule unapotakiwa
kupeleka mawasiliano ili kuboresha zaidi huduma za mawasiliano",alisema
Nyalla.
Miongoni
mwa maazimio yaliyofikiwa na washiriki wa mkutano huo ni pamoja na
kulipa tozo kwa mujibu wa sheria,maombi ya mnara kwenye maeneo husika
ufanywe na watoa huduma za radio na TV kupitia wawakilishi waliopo
katika mkoa husika na mnara unapoanzishwa utumike kwa watoa huduma
watakaohitaji kwa kulipia ghrama za umeme na ulinzi na UCSAF ujikite
kutoa elimu ya mfuko na wajibu wa watoa huduma za mawasiliano.
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF) akizungumza wakati akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano
Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio, Televisheni, watoa
huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma ya maudhui mtandaoni
ulioandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na UCSAF uliofanyika leo Agosti
31,2020 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi
Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote
(UCSAF) akizungumza katika Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya
Ziwa.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph akielezea kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na UCSAF.
Kaimu Katibu wa UCSAF ,Ipyana Jengela akitoa mada kuhusu uanzishwaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote na malengo ya mfuko huo.
Mkuu
wa Idara ya Uendeshaji UCSAF, Albert Richard akielezea kuhusu miradi
mbalimbali inayotekelezwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Wadau wa
mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwemo wamiliki wa vituo vya Radio,
Televisheni, watoa huduma za usafirishaji wa vifurushi na watoa huduma
ya maudhui mtandaoni wakiwa kwenye kikao kilichoandaliwa na TCRA na
UCSAF.
Mjumbe wa Bodi ya UCSAF, Samweli Nyalla akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu
wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi
ya UCSAF akiwahamasisha watoa huduma za mawasiliano kuungana kuomba
ruzuku kujenga minara ili kuongeza usikivu wa vyombo vyao vya habari
kwenye maeneo yasiyosikika. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala
UCSAF, Pius Joseph. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji
UCSAF, Albert Richard akifuatiwa na Kaimu Katibu wa UCSAF ,Ipyana
Jengela.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala UCSAF, Pius Joseph akizungumza ukumbini.
Mkurugenzi
wa Malunde Media 'Malunde 1 blog' , Kadama Malunde (kulia) na Estomine
Henry kutoka Shinyanga Press Club blog wakiwa ukumbini.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakisoma vipeperushi vya UCSAF.
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Maafisa wa TCRA Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment