TANZIA: Mzee Hassan Nassor Moyo afariki dunia - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 18, 2020

TANZIA: Mzee Hassan Nassor Moyo afariki dunia

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya Visiwani Zanzibar na mmoja wa waasisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Mzee Nasoro Moyo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo saa saba katika

Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.


Mwili wa marehemu tayari umekwisha kusafirisha kwenye uwanja wa ndege

Mkoani Tanga na kuelekea visiwani humo na mazishi yake yanatarajiwa

kufanyika leo Jioni kwenye eneo la Fuoni Unguja kisiwani Zanzibar.


Akizungumza jana Mtoto wa Pili wa Marehemu Moyo,Mohamed Moto alisema kwamba mwili wa baba yake ulisafirishwa leo saa tatu asubuhi kwa ndege na kufikishwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya mazishi.


 Mohamed ambaye pia ni katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya

Muheza alisema baba yake alikimbizwa hospitali ya Bombo usiku wa

kuamkia jumanne Agosti 17 mwaka huu kutokana na kuugua ghafla kifua na

kubana pumzi ambayo haikuwa ikitoka vizuri.


“Baba hakuwa akiugua na hakuugua kwa muda mrefu…alianza kubanwa na

kifua na baadaye akaanza kupata shida ya kupumua ilipofika saa 7.00

usiku ndipo akafariki”alisema Mohamed.


Alisema Mzee Moyo atazikwa leo jumanne saa 10.00 jioni nyumbani kwake

Fuoni Zanzibar.


Inna lillah wainna ilayhi rajiuna.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad