HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 27, 2020

SPIKA JOB NDUGAI APITA BILA KUPINGWA UBUNGE JIMBO LA KONGWA

 

 Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Agosti 26, 2020 ametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kupitia msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kupita bila kupingwa katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kongwa.

Akitangaza matokeo hayo kwenye ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Kongwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Dkt. Omary Nkullo amesema Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Ndugai ndiye pekee aliyekidhi vigezo vilivyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kumfanya kupita bila kupingwa.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa amepita bila kupingwa, Mheshimiwa Ndugai amesema anawashukuru wana CCM, viongozi na wanachama kwa ujumla  kwa heshima waliyompatia na kumwezesha kupita bila kupingwa.

“Nahaidi kila haina ya ushirikiano kwa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na kuhakikisha uchaguzi wa Jimbo la Kongwa unaenda vizuri, kwa amani na salama”alisema Spika Ndugai

Pia, Mheshimiwa Ndugai ameahidi kuwa ataendelea kuwa mtumishi wa wanaKongwa na kuwa mwakilishi wao katika maeneo mbalimbali.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akabidhiwa barua ya kupita bila kupingwa katika jimbo la Kongwa kwa nafasi ya Ubunge na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Dkt. Omary Nkullo ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kongwa leo Mkoani Dodoma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad