HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 24, 2020

SHIRIKA LA WORLD VISION TANZANIA LATUMIA SH. BILIONI 8.4 KUKAMILISHA MIRADI SINGIDA

 

 Meneja wa Shirika la World Vison kanda ya Kati,  Faraja Kulanga akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za kufunga mradi wa Kisiriri-ADP.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia wananchi. 
 Mkuu wa Mkoa Dkt Rehema Nchimbi akitembelea mabanda ya Wanufaika wa mradi wa Kisiriri-ADP.
 Wanufaika wa mradi kwenye upande wa elimu wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi, uoni hafifu na ulemavu wa viungo wakiwa wanafuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye  sherehe hizo.
 Wa kwanza kulia ni Afisa Habari wa World Vision kutoka Makao Makuu, Agness Mwafifi, akiwa  na Afisa Habari wa Mkoa wa Singida,  John Mapepele wakiwajibika.
  Wanufaika kwa upande wa kilimo wa mradi wa Kisiriri-ADP wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye baadhi ya mabanda yalipo kwenye sherehe za mabidhiano ya mradi. 
Sherehe ikiendelea.

Na Ismail Luhamba, Singida  
SHIRIKA la World Vision Tanzania kupitia wafadhili kutoka Uingereza limetumia zaidi ya shilingi bilioni 8.4  kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuboresha sekta za Elimu, Afya, Maji, Usafi wa mazingira na kuongeza uchumi wa kaya pamoja na usalama na ulinzi wa mtoto katika kata tano za Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Akitoa taarifa ya kufunga mradi ADP–Kisiriri ulioanza mwaka 2003, Meneja wa Shirika hilo Kanda ya Kati,  Faraja Kulanga, amesema pamoja na kumalizika kwa ufadhili wa shughuli katika kata za Kidaru, Tulya, Kisiriri, New Kiomboi na Old Kiomboi lakini bado wanatafuta miradi mingine, Katika kipindi cha miaka 17 ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali, Mradi huo wa Kisiriri-ADP umeweza kuwafikia na kubadilisha maisha watu zaidi ya 37,000 wakiwemo watoto 4,800. 

“Naishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali sisi pamoja na wafadhili wetu wa Uingereza kuwa ni sehemu ya kuchochea maendelo kwa  wananchi wetu  hapa nchini natumaini kwa miaka hii 17 tuliyokaa tumefanya kazi kwa weledi mkubwa ndio maana  tumeleta mabadiliko makubwa kwenye sekta zote tumezigusa kwa karibu sana, mimi nawatakia kila la kheri wananchi wa kisiriri na kata zote tulipokuwa tukitekeleza mradi huu, tutarudi tena kwa miradi mingine” alisema Kulanga. 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi wa Kisiriri kutosikitika kutokana na Shirika la World Vision kuondoka kwa kuwa tayari limewajengea uwezo wa kutegemea kupitia Serikali hii ya awamu ya tano tunawashukuru sana kwakua nanyi kwenye kusukuma maendeleo ya wana Singida na watanzania pia. 

“Hatupaswi kunungunika kutosikitika kikubwa hapa tunatakiwa kuwashukuru sana World Vision kwa miaka yote 17 kuwa na sisi inatubidi kuvitunza, kuvilinda na kuvithamini hasa kwa umakini mkubwa sana na kutumia maarifa tuliyo achiwa na wadau wetu wa maendeleo kuviendeleza zaidi maana kama maarifa wametuachia yakutosha  ”.alisema Nchimbi.

Baadhi ya wananchi walionufaika na mradi huo wanakiri kuleta mabadilko makubwa katika maeneo yao hasa kwenye Elimu Afya Mazingira na Maji na kwa watoto wetu pia tunawashukuru kwa kujitowa kwa ajili yetu na sisi tunaahidi kuyaendeleza yote yaliyo mema na kutumia ujuzi mlio upandikiza kwetu kwa muda wote wa miaka 17 .

Katika miaka 17 hiyo mradi umeweza kuchimba visima (5) na visima vifupi (10) katika vijiji vyote vya eneo la mradi, kwa kushirikiana na Halmashuri ya Wilaya ya Iramba wamefanikiwa kusambaza mifumo ya maji katika Kijiji cha Meli na Hospitali ya Wilaya ya Iramba. 

Kwenye upande wa elimu mradi umefanikiwa kujenga madarasa (19) katika shule ya msingi Ndurumo 7, Migilango 3, Doromoni 1, Kisiriri 4, Mampanta 2 na Kinambeu 2.Tumeweza kujenga nyumba 8 za walimu katika shule za msingi Ndurumo 2, Dolomoni 1, Kisiriri 2, Migilango 1, Mampanta 1, Kinambeu 1 na ofisi 2 za walimu zilijengwa, hayo ni baadhi tu mafanikio ya Kisiriri-ADP.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad