HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 12, 2020

GEREZA ROMBO WAPATIWA MAFUNZO YA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU MAGEREZANI

 Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Hassan Mkwiche akiwasili leo Agosti 11, 2020 katika Gereza la Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro akiwa ameongozana na msafara wa Timu ya wataalam(hawapo pichani)kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya. Kushoto kwake ni Mkuu wa Gereza Rombo, ASP. Lucas Mboje.

 Mkuu wa Gereza Rombo, ASP. Lucas Mboje akiwa ameongozana na Timu ya wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya ambao leo wameendesha Mafunzo ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu magerezani kwa maofisa na askari wa Gereza Rombo.
 . Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Hassan Mkwiche(katikati) akitoa maelezo mafupi kabla ya kuwakaribisha wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya kutoa mafunzo ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu magerezani kwa maofisa na askari wa Gereza Rombo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi kutoka  Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya(kushoto) ni Dkt. Wilbard Mhandiki.
 Mtaalam kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Emmanuel Matechi akitoa historia ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa washiriki.
 Maafisa na askari wa Gereza Rombo wakifuatilia mafunzo ya kudhibiti kifua kikuu magerezani.
Timu ya wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya wakifuatilia mafunzo hayo.
  Washiriki wa mafunzo ya kudhibiti kifua kikuu magerezani kutoka Gereza Rombo wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam  kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya leo mara baada ya mafunzo leo Agosti 11, 2020(Picha zote na Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad