Mgombea
Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi (kulia)
akikabidhiwa fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi na
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mkuu Mstaafu Hamid
Mahmoud (ZEC) Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali
Mwinyi (kushoto) akiwapungia mkono umati wa wana CCM waliojitokeza
kumsindikiza kuchukua fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC).
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali
Mwinyi (kushoto) akiwapungia mkono umati wa wana CCM waliojitokeza
kumsindikiza kuchukua fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC).
Baadhi ya wana CCM waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali
Mwinyi akiwa amembeba mmoja wa watoto waliojitokeza pamoja na wana CCM
kumsindikiza kuchukua fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC).
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali
Mwinyi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya
kukabidhiwa fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC).
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali
Mwinyi (katikati) akisalimiana na wana CCM waliojitokeza kumsindikiza
kuchukua fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC).
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali
Mwinyi (katikati) akisalimiana na wana CCM waliojitokeza kumsindikiza
kuchukua fomu za kugombea Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC).
Na Joachim Mushi, Zanzibar
MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.
Hussein Mwinyi leo ameisimamisha Zanzibar na viunga vyake alipojitokeza
kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa nafasi ya urais wa Zanzibar katika
Ofisi za Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Maisara.
Mgombea huyo ambaye tayari ameahidi neema ya ajira kwa vijana ikiwa
ni utekelezaji wa sera ya chama hicho iliyowekwa mwaka 2020-2025
itakayoleta ajira takribani 300,000 kwa Vijana, amezindikizwa na mamia
ya wanachama na vijana waliokuwa katika maandamano yake.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la Tume baada ya
kukabidhiwa fomu yake na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
Jaji Mkuu Mstaafu Hamid Mahmoud ameahidi kulisimamia suala hilo kipekee
ili kupunguza kero ya ajira.
Dk Mwinyi alisema miongoni mwa vipaumbele vyake ambavyo vinatokana na
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025, ni kuimarisha
sekta ya viwanda, utalii na uvuvi wa bahari kuu kwa ajili ya kuzalisha
nafasi za ajira, ambapo amekusudia kutekeleza sera na ilani ya chama
hicho kwa vitendo kama watangulizi wake.
“Mimi kama mgombea wa Chama Cha Mapinduzi nitainadi ilani hiyo ya
ajira 300,000 lakini lazima vijana tuwaandae tuwape mafunzo tuwe na vyuo
vya utalii, vyuo vya uvuvi ili vijana wawe weledi, nataka niwaambie
vijana wakae tayari kuingia katika soko la ajira wawe tayari kufanya
kazi,”
Alibainisha kuwa tayari mikakati imewekwa katika kuwaandaa Vijana
kuingia katika soko la ajira kwa kuimarisha Vyuo vya utalii, pamoja na
Uvuvi ambavyo vitawaandaa Vijana kuweza kuvua katika uvuvi wa bahari
kuu.
“Natambua kuna changamoto nyingi zinazowakabili vijana lakini lazima
tukuze uchumi, lazima tuwe na sekta za vipaumbele ukitizama eneo la
utalii, suala la uvuvi, suala la viwanda hayo maeneo tukiyafanyia kazi
sina shaka tutaongea idadi ya uajira kwa vijana wetu,”
Aidha akizungumzia kuhusu kukuza uchumi, alibainisha kuwa hatokuwa
tayari kuachia rushwa ifanyike chini ya utawala wake na wale wote ambao
wana tabia ya kukwepa kodi basi wajue kwamba hawatopata nafasi chini ya
serikali yake ambayo amekusudia kuiongoza iwapo atapata ridhaa ya
kuongoza katika kipindi chake.
Pamoja na hayo aliwataka wapinzani wa CCM kutambua kuwa chama hicho
hakijagawanyika baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni, bali
kipo vizuri kiushirikiano na wagombea wote walioshiriki katika mchakato
wa awali.
''Viongozi wenzangu katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu
nawaomba tusubiri wakati ufike tutafanya kampeni za kistaarabu sana
zenye amani na utulivu kauli ambazo zitakuwa na lengo la kuwaunganisha
wananchi na sio kuwagawa kwa kuwabaguwa ''alisema mgombea huyo.
Awali akimkabidhi fomu ya ugombea, Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu
mstaafu Mahmoud alimueleza mgombea huyo masharti yanayopaswa kufuatwa
yalioandikwa kwenye fomu hizo.
“Ili mtu ateuliwe na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuwa mgombea
nafasi ya urais awe na sifa ya kugombea, achukue na kujaza na kurejesha
fomu ya uteuzi iliyotayarishwa na tume ya uchaguzi kabla ya muda
uliowekwa Tume, na fomu ya uteuzi iliyojazwa na mgombea iwasilishwe
pamoja na maelezo binafsi ya mgombea kama inavyohitajika kutolewa kwa
mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa pamoja kuwasilishwa hati ya kiapo
katika muda uliwekwa iliyojazwa na kutiwa saini za wadhamini wa mikoa
yote ya Zanzibar pamoja na picha nne zilizopigwa miezi mitatu nyuma
kabla ya uteuzi”. Alisema Mwenyekiti wa ZEC. Jaji Mkuu MstaafuHamid
Mahmoud.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk. Abdalla Juma Sadalla
(Maabodi) aliwataka wanachama na wafuasi wote wa chama cha Mapinduzi
kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28
ili kukipa ushindi chama hicho kwani bila ya kupigwa kura kwa wingi
hakuna ushindi.
''Nikwambieni hivi njia pekee ya kupata ushindi wa kishindo katika
uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2020 ni kwa wanachama na wafuasi
kujitokeza kwa wingi kumpigia kura mgombea wetu Dk Hussein Mwinyi na
kumfanya kuwa rais wa Zanzibar, kwa hivyo siku ikifika mjitokeze kwa
wingi sana kwenda kumpigia kura yeye na wabunge wetu na wawakilishi
pamoja na madiwani,'' alisema Naibu huyo.
No comments:
Post a Comment